Ili kuongeza ushindani katika soko la kimataifa la zao la tumbaku na  kampuni za ununuzi wa tumbaku nchini ,wakulima wa tumbaku kutoka chama kikuu cha ushirika Kahama (KACU) wameziomba taasisi za kifedha kutoa mikopo kwa chama hicho ili kiweze kununua zao hilo kwa msimu wa mwaka 2021/22.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na www.simamia.com jana katika mkutano mkuu wa 25 wa chama hicho baadhi ya wajumbe wa mkutano huo,Makenzi Nkunda kutoka Amcos ya Jitegeme alisema kuwa mwaka jana zaidi ya kilo 2000 za tumbaku zilikosa mnunuzi na wakulima kulazimika kupata hasara baada ya kuja kununuliwa kwa bei ya ndogo.
Alisema kuwa kama mwaka jana benki ya Kilimo (TADB) iliweza kutoa mkopo kwa KACU kwaajili ya kununulia zao la pamba ambapo mkopo huo ulileta matokeo chanya kwa wakulima wa zao hilo ambapo waliuza mazao yao kwa bei nzuri ambayo ilileta ushindani baina yao na kampuni zinazohusika na ununuzi wa zao hilo.
âTunaziomba taasisi zingine za kifedha hapa nchini kutoa mikopo kwa KACU ili kiweze kununua tumbaku kwa msimu wa kilimo wa mwaka huu,wakulima tunazalisha kwa kuzingatia viwango vya kimataifa lakini mwisho wa siku tunakosa masoko,endapo kama chama chetu kinanunua zao hili kutoka kwa wakulima sisi tutanufaika,âalisema Nkunda.
Joseph Nganiki ni mkulima kutoka Amcos ya Saweka alisema kuwa kila mwaka wakulima wa tumbaku lazima wakumbane na tatizo la kukosa masoko ama kukosa mnunuzi hali ambayo imekuwa ikiwakatisha tamaa kuendelea kulima zao hilo ambalo linaliingizia taifa fedha nyingi za kigeni.
âEndapo KACU itaanza kununua tumbaku tutaweza kuondokana na tatizo la wakulima kukosa wanunuzi pindi wanapotaka kuanza uzalishaji,benki zetu zitusaidie kutatua changamoto hii kule vijijini watu wanapata shida sana baada kulima na baadae wanakosa mnunuzi,âalisema Nganiki.
Akilitolea ufafanunzi suala hilo Meneja kitengo cha kilimo na biashara wa benki ya (CRDB) Richard Tarimo alisema kuwa benki hiyo inaendelea kutoa mikopo mbalimbali kwa vyama vya msingi mbalimbali hapa nchini ambapo kwa msimu uliopita walitoa mkopo wa dola za kimarekani milioni 30 kwa wakulima wanaodhalisha zao la tumbaku.
âCRDB itaendelea kutoa mikopo kwa AMCOSÂ na kama KACU wataamua kwenda kununua tumbaku msimu huu ni lazima waje na vielelezo vinavyotakiwa ikiwa ni pamoja na mkataba wa unununuz kutoka kampuni za njeWS zitakazonunua zao hilo na watapatiwa mkopo kwa njia rafiki,âalisema
Kwa upande wake mwenyekiti wa KACU Emmanuel Charahani alisema kuwa wazo hilo watalifanyia kazi kwa ukaribu lakini muda si mrefu chama hicho kitazindua kamapuni mpya ya ushirika kampani limited ambayo itajiendesha kibiashara hivyo wakulima hao wasiwe na wasiwasi.
âKampuni yetu mpya tumelenga kuiendesha kibiashara ili kuhakikisha inaleta matokeo chanya ikiwa ni pamoja na kusimamia kwa ufanisi mkubwa miradi yote inayotekelezwa na KACU sambamba na kutoa ajira kwa wakulima wetu,âalisema Charahani.
Recent Comments