SALVATORY NTANDU
USHETU
22/2/2021
Wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini (TASAF) katika halmashauri ya Ushetu wilayani kahama mkoani Shinyanga wameomba kuondolewa katika mpango wa kupokea fedha za ruzuku baada kujikwamua kiuchumi ili kuwapa fursa watu wengine kupatiwa ruzuku hiyo ambayo itawasaidia kuondokana na hali ya umasikini.
Wananchi hao wameieleza hayo www.simamia.com juzi baada ya kutembelewa na maafisa wa Tasaf kutoka makao makuu,ambao wanapita katika kaya zao kujionea namna wanavyotumia fedha za ruzuku zinazotolewa na serikali ili kuzikomboa kaya masikini kwa lengo la kijikwamua kiuchumi..
Merry Michael Nonga mkazi wa Uyogo katika halmashauri hiyo alisema kuwa hapa awali maisha yake yalikuwa magumu kwani alikuwa akiishi na watoto wake katika nyumba ya nyasi lakini baada ya kuingizwa katika mpango huo amefanikiwa kujenga nyumba ya kisasa na kusomesha watoto kwa ngazi ya shule ya msingi hadi chuo kikuu.
âTasaf imenisaidia mimi kubadili maisha yangu,kwa sasa mimi ni tajiri ajaye ninangâombe wawili wa kulimia mashamba yangu,nimejenga nyumba ya kisasa,ninafuga mbuzi,kondoo na kuku na mwaka huu natarajia kuvuna nguni za mpunga zaidi ya 50 kwa mafanikio haya naishukuru serikali na pia naomba kuondolewa katika mpango huu,âalisema Nonga.
Magreth Bundala  mkazi wa Uyogo alisema kuwa tangu ameanza kupokea fedha za ruzuku ya Tasaf amefanikiwa kujenga nyumba mbili za kisasa ambazo zinamsadia kupangisha watu wengine na kisha yeye kujipatia fedha ambazo zinamsaidia kuendesha familia yake.
âkwa sasa nasomesha watoto wangu wawili katika ngazi ya elimu ya juu kupitia fedha za ruzuku hii kipekee naipongeza serikali kupitia Tasaf kwa kutubadilishia maisha sisi wananchi wanyonge ambao hapo awali tulikuwa tunaishi maisha ya ufukara,ninaomba kuondolewa katika mpango huu ili kuwapa fursa watu wengine wanufaike kama mimi,âalisema Bundala.
Lule John ni mmoja wa wanufaika wa mpango huo alisema kuwa amefanikiwa kulima shamba la michungwa ekari mmoja ambayo muda si mrefu ataanza kuvuna matunda na fedha alizotumia kununulia miche ni za ruzuku ya Tasaf ambayo anaendelea kupatiwa na serikali.
âNatarajia kuvuna gunia zaidi ya 50 za machungwa ambazo zitanisaidia kupata fedha zaidi ya shilingi milioni mbili ambazo msimu wa kiangazi natarajia kuanza bishara ya kuunza nguo na duka la reja reja amabalo litasaidia mimi na familia yangu kuuaga umasikini,âalisema John.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Tasaf makao makuu Zuhura Mdungu aliwaponge wanaufaika wa mpango huo kwa kujikwamua kiuchumi hasa kwa kuanzisha miradi ya kiuchumi ambayo imesaidia kukuza vipato vya familia zao sambamba na kuwapeleka watoto wao shule.
âNiwaombe waratibu wa Tasaf kila wilaya waendelee na zoezi la uhakiki walengwa ambao watabainika kukosa sifa waondolewe kwenye mpango ni sisi tunajivunia kuona kunawatu wamebadilika kutoka katika hali ya ufukara hadi kuwa matajiri wajao,niwapongeze kwa kuthubutu endeleeni kufanya kazi za kulijenga taifa letu,âalisema Mdungu
Mwisho
Recent Comments