Na, Juventus Juvenary
Siku 5 baada ya Kada wa CCM Baraka Bitariho, mzaliwa wa Kabanga wilayani Ngara kutangaza nia ya kugombea ubunge wa jimbo la Ngara, baadhi ya wananchi wilayani humo wamemtaka kushghulikia changamoto mbali mbali zinazowakabili
Itakumbukwa www.simamia.com juai 8 mwaka huu ilichapisha habari ikimnukuu Baraka Bitariho ambaye alitangaza nia akiwa Marekani kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu uatakaofanyika Oktoba kwaka huu na habari hiyo ilieleza historia yake âKwa wanaomfahamu zaidi nyumbani anajulikana kama Bhankâanzako ama kwa kifupi, Bankaâ.
Historia yake kitaaluma inaanzia katika Shule ya msingi Nzaza, Baba yake mzazi  anatokea kijiji cha Murukukumbo, na mama anatokea Nzaza. Kitaaluma, Baraka Bitariho ni mtalaam wa Sheria na Uchumi. Ana shahada ya Umahiri ambayo kwa kimombo huitwa (masters in Business administration)
Ni miongoni mwa watia nia kugombea Ubunge wa Jimbo la Ngara akilenga kulikwamua jimbo hilo katika sekta mbalimbali kuelekea katika maendeleo ya Viwanda kwakushirikiana na wananchi kuungana na Serikali kufikia malengo ya Uchumi wa kati
Nimezungumza na Baraka Bitariho kuhusu dhamira yake kugombea Ubunge nikitaka kufahamu msukumo wake katika maendeleo ya jimbo, na kwanini yeye achaguliwe kuwa mbunge kupitia Uchaguzi mkuu wa Oktoba tofauti na watia nia wenzake ambao kwasasa wanakaribia 40!
Yafuatayo ni majibu yake ambayo yanaambatana na vipaumbele:-
â Ningependa kuleta miundo mbinu kwa wana Ngara. Natamani kupitia uongozi wangu, Ibaki historia kubwa ya maboresho na ujenzi wa miundombinu mbali mbali katika jimbo letu. Ni Ukweli kuwa licha ya rasilimali nyingi na muhimu zilizopo Wilaya ya Ngara bado,wananchi wanakabiliana na changamoto za miundombinu hasa Maji,Umeme,barabara nk. Nikifanikiwa kupewa ridhaa nitashughulikia changamoto hizo
-Nitashughulikia matatizo yanayowakabili Vijana. Natambua kuwa Vijana ni kundi muhimu sana katika mustakabali wa Nchi. Vijana ni kundi muhimu na kubwa ambalo wakati mwingine linaitwa Nguvu kazi ya Taifa. Vijana bado wanakabiliwa na changamoto ya Ukosefu wa ajira na shughuli nyingi za kuingiza kipato. Nikiwa Mbunge nitafuatilia upatikanaji wa mikopo na fursa za kuwaendeleza
-Hatuhitaji kukimbilia Dar es Salam ama majiji makubwa kutafuta Kazi na vibarua. Kumekuwa na kasumba ya wana Ngara kukimbilia katika miji Mikubwa hasa Dar es Salaam, Mwanza,Arusha Mbeya na kwingineko. Hali hiyo inaididimiza Ngara kwakuwa walio wengi wakishafika huko hawarudi kujenga na kuiendeleza Ngara. Naamini kwakushirikiana na watalaam, utekelezaji mzuri wa Ilani na Sera za Nchi tutafanikiwa kujenga miundombinu, kuboresha huduma na kuwafanya wananchi wentu kuipenda Ngara kisha kuamua kuwekeza na kujenga pasipokulazimika kuhamia miji mingine kufuata huduma
-Tumalizapo shule huku Ngara inatuhitaji. Ni wakati wakuunganisha watu waliofanikiwa kusoma, nikiwa Mbunge nitawahamasisha Viongozi,watumishi wa serikali,mashirika na asasi nyinginezo kuwa wazalendo. Tumalizapo Shule turudi kuijenga Ngara.
-Nitasisitiza na kujenga uchumi wa Ngara unaoegemea teknolojia. Ni ukweli usiopingika kuwa Ngara imejaaliwa kuwa na vipaji vya hali ya juu. Ina wananchi wabunifu na wenye moy wa kulitumikia Taifa. Nikiwa Mbunge wa Jimbo hili lenye utajiri wa kila aina, nitatumia nafasi yangu kuhakikisha Uchumi wa Ngara unainuka na kuwekeza zaidi katika teknolojia. Nitashirikiana na wahisani,wawekezaji na kuishawishi Serikali kujikita katika Viwanda na kwakutumia Teknolojia itakayowafaidisha wananchi hasa vijana. Mfano, Tunaweza kutafuta namna ya kukaribisha wawekezaji kutoka mataifa yaliyoendelea kiviwanda,kushirikiana na wawekezaji wa Ndani pamoja na wafanya biashara wazawa kuanzisha viwanda vya kuunda na kutengeneza Pikipiki,Magari,Vipuri na zana za Kilimo
-Ngara inahitaji fikra mpya na zinazotekelezeka. Tumechoshwa na ahadi zisizotekelezeka. Ninajiamini na nategemea nitakaposhinda kuwa Mbunge wa Jimbo la Ngara nitatumia uzoefu wangu na maarifa niliyonayo kuhakikisha tunaondokana na dhana zilizozoeleka ambazo zimeshindwa kuisogeza Ngara hasa Kilimo na Mifugo ya mazoea tangu taifa limepata Uhuru, ili kuleta maendeleo
-Kero za Mipakani.watanzania wenzangu hasa wapiga kura wa jimbo la Ngara, tumekuwa na kero ambayo kwa namna moja ama nyingine imekuwa kikwazo cha Maendeleo. Nitahakikisha tunaondokana na unyanyasaji unaowakumba wananchi wa Mipakani kwakufananishwa na raia wa kigeni wanaoingia Nchini bila kibali wala ruhusa za mamlaka husika. Tumeshuhudia usumbufu mkubwa unaofanywa na Idara za Uhamiaji, Jeshi la Polis na mamlaka nyingine kwa wananchi pale wanapolazimika kukamatwa,kuwekwa ndani na kukoseshwa haki zao za msingi. Inakuwaje leo, Raia wa Ngara alazimishwe kutoa vibali kwakudhaniwa ni raia wa kigeni hasa nchi jirani?
Hali hiyo inakosesha fursa watu wengi hasa wanapofika kwenye Ofisi na mamlaka zinazotoa huduma mbali mbali hasa udhamini wa masomo na vibali vya safari za nje. Hii ni Kero na nimedhamiria kuiondoa
Na kwakuongezea hili, nitaishawishi serikali isogeze huduma karibu kwakujenga Vituo vinavyotoa vitambulisho vijengwe Ngara ili vijana wetu wapate kazi, sio mtanzania alazimike kusafiri umbali mrefu kwenda mikoa na majiji ya mbali kupata kitambulisho huku Mwana Ngara angefanya kazi vizuri tuu akiwa jimboni kwangu, Ngara.
-Baadhi ya Viongozi wengi tuliowachagua wamekuwa Mabubu. Wengi wamesahau dhamana waliyopewa na wapiga kura na kujifanya hawazioni changamoto za wana-Ngara na wala hawajishughulishi kuzitafutia ufumbuzi. Watu wanamna hiyo hawafai na ninafasi kwa mpiga kura kutowapa nafasi wala dhmana ya uongozi tena kwa maana ya kuwa tumewaona na kuwashuhudia hawajali, wamekuwa watu wa kujali maslahi yao na kutetea mishahara yao tu.
Mfano mzuri, Miezi kadhaa iliyopita tulishuhudia mgomo wa madareva wa Malori katika mipaka yetu na Nchi jirani hasa Kabanga-Kobero-Burundi ,na Rusumo-Rwanda, Mtoto kutumbukizwa chooni,Mikatiko ya Umeme ya mara kwa mara, Changamoto za Uhamiaji, Ubovu wa Barabara, na mengine mengi ila Mbunge anayemaliza muda wake hakusema chochote utadhani hakuyaona wala kusikia.
-Vijana wetu wanashinda barabarani wakiendesha Pikipiki, ila wanasumbuliwa, na wakati mwingine wengine wakipoteza maisha katika matukio yanayowahusisha Askari wa jeshi la Polisi hasa kitengo cha usalama barabarani. Kwa dhamira ya dhati kabisa niko tayari kushirikiana na wananchi wenzangu wa Jimbo la Ngara kuhakikisha tunapata suluhisho la changamoto na Usumbufu huo
-Ngara imebarikiwa kuwa na Mapori, ardhi nzuri na mazingira safi yanayohamasisha Kilimo na mifugo. Wafugaji wanaonewa na wengine wanasondekwa ndani na Polisi wanaotaka rushwa. Â Wana-Ngara wananyanyaswa na wale tuliowapa ridhaa ya uongozi. Hii hali haitokubarika ikiwa mimi Baraka Bitariho nikiwa kiongozi wenu kama Mbunge wa jimbo la Ngara. Najulikana kama âGUKANZAKOâ nikiwa na maana ya Mtu anayefanya utatuzi wa jambo haraka. Jimbo la Ngara linahitaji mbunge mwenye maamuzi ya haraka katika kutatua kero na kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya Wananchi. Mimi naweza
-Nina imani Mheshimiwa rais wetu Dkt.John Pombe Joseph Magufuli atapewa ridhaa tena ya Miaka 5 kukamilisha utawala wake wa mhula wa pili wa awamu ya 5. Niko tayari kushirikiana naye kuhakikisha Watanzania wanafurahia matunda ya Serikali yao. Naomba wananchi wenzangu waniamini na wanipe ridhaa ya kuwaongoza
Katika uongozi wangu, furaha yangu itakuwa ni kuwaona Wanaotafuta na kwa jasho lao walindwe na kuheshimiwa. Tuwawaajibishe walinzi wa nchi hii hasa Polisi watekeleze majukumu yao ipasavyo kuwalinda raia na Mali zao na si kuungana na waovu kupora jasho letu . naomba wana Ngara waniamini kuwa mimi Baraka Bitariho nitaleta miundo mbinu ya kiuchumi ili hata wale wasiobahatika kuendelea na shule wapate kazi au mafunzo yatakayowawezesha kujikimu kiuchumi
Naamini na naomba kuwaeleza wapiga kura kuwa, mimi kama mfanya biashara na mwanasheria, nia yangu ni kuleta  mchango mkubwa kimaendeleo na ahidi pia kushirikiana na viongozi wa kitaifa na kimataifa katika uendelezaji wa nchi yetu.
Naomba kuwashukuru,nikiamni mtanipa kura kupitia Uchaguzi mkuu. Chagua CCM, Chagua Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Chagua Mbunge Baraka Bitariho kwa Maendeleo ya Ngara.
www.simamia.com / na Simamia Tv tunamtakia Kila Lakheri katika Uwakilishi wa jimbo la Ngara.
Unaweza kutangaza nasi,kuchapisha habari na kurusha taarifa zako kwakuwasiliana nasi kupitia simu na whatsapp 0756432748
Kupitia play store,Pakua App yetu Simamia tv install kwenye simu yako kwaajili ya Kupata habari kila wakati.
Recent Comments