Mwanasheria maarufu nchini Tanzania, Alberto Msando amefunguka kuwa Wasanii wa Tanzania huu ni muda wao muafaka wa kujitambua na kujithamini kwa kukaa siti ya mbele katika kushiriki kwenye vikao na mikutano inayojadili kwa upana masuala ya haki zao na sio kulalamika tu.
Msando amesema hayo jana kwenye kikao maalumu kilichoitishwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kilichoongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Harrison Mwakyembe kwa lengo la kujadili namna ya kutatua changamoto za Wasanii.
âWasanii lazima waache uzembe na kujisahau suala la kupigania haki zao suala la kuboresha kazi zao ni la kwaoâ¦.Ni wakati wao hao kama wasanii kukaa siti ya mbele katika kupigania haki zaoâ,amesema Msando.
Hata hivyo Msando amewaasa Wasanii kushiriki vya kutosha kwenye mijadala na mikutano mbalimbali inayowahusu hao ili kuongeza uweledi katika kuboresha sanaa na kujua haki zao msingi.
â¦Waziri Mwakyembe aunda Kamati ya kujadili namna ya kutatua changamoto za Wasanii (+Video)
Kitu cha kushangaza kwenye kikao hicho Wasanii ambao ndiyo wahusika wakuu mahudhurio yao yalikuwa mabovu ukilinganisha na Wadau na Waandishi wa Habari walioitikia wito huo.
Recent Comments