Recent Comments

WASICHANA WAOGESHWA DAWA ZA MAPENZI KUWAVUTIA WANAUME

By Simamia Journal Oct 7, 2020

WANANCHI wa Halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga, wamekuwa na tabia ya kuwapeleka watoto wao wa kike hasa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wenye umri wa kuanzia miaka 16 hadi 18 kwa waganga wa jadi kuwaogesha dawa za mapenzi za kuwavutia wanaume ili waolewa haraka.

Moja ya sababu ya kuwapeleka kwa waganga wa jadi kuwaogesha dawa za mapenzi ni kutaka watoto wao kuoelewa mapema baada ya kupevuka ili asije akaharibika akiwa mikononi mwa wazazi wake na baadae kuja kukosa mahali ya ng’ombe.

Waliyabainisha hayo jana wakati wa warisha ya siku mbili ya maandalizi ya ujenzi wa nguvu ya pamoja katika kuimarisha mila na desturi chanya katika jamii zinazohusu wasichana iliyoshirikisha washiriki kutoka kata za Shilela na Lunguya kwa ufadhiri wa mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP).

Lameck Kanyefu,mkazi wa kata ya Shilela alisema,mbali na kuwaogesha dawa za mapenzi,wamekuwa wakichanjwa chanjo mwilini za mvuto wa mapenzi ili anapohitimu elimu ya msingi au sekondari aweze kupata mchumba na kuolewa na wengine wamekuwa wakiolewa kabla ya kumaliza masomo.

“Msukuma anathamini sana ng’ombe kuliko kitu chochote kile,wakati wa mahali ya kumwoza binti yake hata ukimpatia Milioni 10 hatajisikia vizuri na ndio sababu ya wafugaji wengi wa jamii yetu kuwaozesha watoto wao kwa mifugo”Alisema Kanyefu.

Nae Hamisa Hamisi aliema,akinababa kwenye familia wamekuwa wakielewa mahali wakiwa kwenye virabu vya pombe na mwisho wa siku unapewa taarifa juu ya binti kuolewa na kwa kuwa kwenye jamii yetu mwanamke hana sauti ya kuhoji unabaki kimya.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa kata ya Lunguya Lusajo Manase alisema kuwa,baadhi ya viongozi hasa Mwenyeviti wa vitongoji na vijiji wamekuwa wakishiriki katika kuwaozesha watoto wa wadogo chini ya miaka 18 kwani wanakuwa wageni rasmi kwenye sherehe za ndoa hizo.

Hata hivyo alishauri viongozi wa madhehebu ya kidini kwenye ibada zao kuendelea kutoa elimu ya madhara ya ndoa za utotoni kwa waumini wao ili wawe mabarozi wazuri kwenye maeneo yao nakwamba ikitokea kitendo hicho awe na hofu ya Mungu na akutoa taarifa kwenye vyombo vya sheria.

Kwa upande wake Mwezeshaji Mwanachama wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Rehema Mwateba alisema,kumuoza mtoto wa kike akiwa na umri mdogo ni kumsababishia hapo baadae kutopata uzazi(ujauzito) baada ya mbengu zinazosababisha mimba kutofika sehemu husika na via vya uzazi kuharibika.

Pia alisema kuwa,vitendo hivyo ukumbwani vimekuwa vikiwakimbiza akinadada wengi kwa waganga wa jadi au wachungaji kwenda kutafuta watoto na kuwataka wazazi na walezi kuwa mabarozi wazuru katika kuridhibiti jambo hili lisiendelee kutokea katika maeneo yao.

Mwisho.

By Simamia Journal

Tangaza nasi. www.simamia.com YouTube Chanel: www.youtube.com/c/SimamiaTv