NA, MWANDISHI WETU
Mfumo wa vyama vingi ni hali ya kuwa na chama zaidi ya kimoja,katika nchi moja.Madhumuni ya kuwa na vyama vingi vya siasa ni kuleta ushindani wa kisiasa,ili kuleta maendeleo ya nchi,upinzani wa kisiasa sio uadui kama watu wengi kwenye nchi zinazoendelea wanavyodhani,kuwa na vyama vingi ni kuongeza wigo wa demokrasia katika jamii ya husika.
Tanzania ni nchi yenye mfumo wa vyama vingi vya siasa uliorejeshwa katika katiba ya Tanzania mwaka 1992.
Hivyo taifa la Tanzania lina vyama kama vile Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho kimetokana na muungano kati yaTanganyika African National Union (TANU) naAfro Shiraz Party (ASP) ya Zanzibar,Civic United Front (CUF),Tanzania Labour Party (TLP),Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),National Convention for Constitution and Reconstruction-Mageuzi (NCCR-Mageuzi),National League of Democracy (NLD),Democratic Party (DP), Demokrasia Makini.
Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) na Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA)Katika ushindani vya vya saisa vinavyo onekama kufukuziana zaidi kwenye ushindani wa kuitaka Ikulu ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwani ndiyo vyama vyenye wafuasi wengi kushinda vyama vingine.
Hata hivyo ushindani huo ni ushindani wenye kuchochea maendeleo kwani kila chama kinajihami kufanya vizuri ili kisishindwe na chama kingine.
Hata hivyo hilo siyo hitaji la watanzania bali hilo ni hitaji la vyama vya siasa, hitaji la wanzania ni kuwa na utawala bora na maisha bora kwa kila mtanzana.
Ninapo zungua mzia utawala bora na maisha bora huu ni ugonjwa wa bara la Afrika kwani nchi nyingi za Afrika zimekosa utawala bora mambo linalo pelekea maisha ya waafrika kutokoa bora kwani vitu hivi vinaenda sambamba.
Leo hii tukiitazama wilaya ya Ngara ni wilaya ambayo ipo mpakani mwa nchi zaidi ya moja ambapo Kuna Mipaka mikubwa mitatu kama vile Rusumo mpakani mwa Rwanda na Tanzania, Kabanga mpakani mwa Tanzania na Burundi, Murusagamba mpakani mwa Tanzania na Burundi huku taifa la Congo likitimia mipaka hiyo ziko fursa nyingi katika wilaya hii lakini bado maendeleo yaliyopo hayalingani na fursa zilizopo.
Ngara haina soko lenye hadhi ya kimataifa hivyo watu kutoka Burundi, Rwanda na Congo hulazimika kufuata bidhaa Kahama, Mwanza, Shinyanga ama Dar es salaam.
Ngara Bado Ina changamoto ya huduma za afya zipo kata hazina vituo vya afya na kuna vijiji havina zahanati.
Ngara haina miundombinu ya maji inayo kidhi mahitaji ya wakazi ambapo wakazi wengi hutumia maji ambayo siyo salama kwa afya zao.
Ngara ina changamoto katika miundombinu ya barabara ambapo mpaka sasa ni maeneo machache ambayo miundombinu hiyo inapitoka vizuri.
Ngara hiana vituo vya mabasi vyenye hadhi ukulinganisha na hadhi ya kuwa na mipaka mitatu mikubwa.
Utawala bora maisha bora kwa kila mtanzana ndilo hitaji lao kubwa la msingi ukweli mtanzania hawezi kujali ni nani anaongoza taifa kama haya mambo mawili akiwa anayapata.
Recent Comments