Wataalamu wanashauri kuwa ni vyema watoto wanaozaliwa na matatizo ya ‘kasoro’ za midomo watibiwe mapema kuanzia miezi miwili.
Ushauri huo umetolewa na Madaktari wataalamu wa upasuaji wa midomo wazi au midomo sungura ambao wameweka kambi kwa muda wa wiki moja ambapo watoto kadhaa waliozaliwa na tatizo hilo watafanyiwa upasuaji Katika mji mkuu wa Tanzania Dodoma.
Huduma hii inayotolewa bure inafanyika kwa ushirikianio wa Hospitali ya Mkoa Dodoma na taasisi isiyo ya kiserikali ya Same Quality Foundation.
Dr. Atenus Masele ambae ni daktari bingwa wa kinywa na meno ameniambia kwamba mwitikio ni mkubwa mkoani Dodoma kwa sababu awali walikuwa na malengo ya kuwafanyia upasuaji watoto 20, lakini mpaka sasa waliojiorodhesha ni zaidi ya hao
Hata hivyo, licha ya kutokuwepo kwa takwimu zinazoonyesha ukubwa wa tatizo la watoto kuzaliwa na midomo sungura, imeelezwa kwamba kanda ya kaskazini mwa Tanzania kuwa na idadi kubwa ya watoto hao.
Recent Comments