Recent Comments

WATU 11 WAFARIKI DUNIA KATIKA MLIPUKO KIWANDA CHA MTIBWA SUGAR

By Simamia Ngara May 23, 2024

NA, MWANDISHI WETU.

Watu 11 wakiwemo raia watatu wa kigeni wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa na kukimbizwa hospitali ya Misheni ya Bwagala kwa matibabu baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme katika kiwanda cha Sukari cha Mtibwa wilayani Mvomero mkoani Morogoro.

Aidha hitilafu hiyo ya Umeme imedaiwa kutokea kwenye mtambo wa kupitisha mvuke wa kuzalisha umeme kiwandani hapo.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama akiwa eneo la tukio amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa saba na nusu, Mei 23 mwaka huu, yaani usiku wa kuamkia leo.

Pia amewataja waliofariki dunia kuwa ni wataalamu wa umeme na mitambo waliokuwa kwenye chumba cha kuendesha mitambo hiyo.