-
WATU 12 WAKAMATWA KWA UVAMIZI WA ENEO LA MWEKEZAJI.
Na Musa Mathias, Â Â mussamathias573@gmail.com
Morogoro.
Watu kumi na mbili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro kwa tuhuma za  uvamizi, uharibifu wa mali pamoja na utoaji wa taarifa za kupotosha kuhusu shamba la Mkonge linalomilikiwa na mwekezaji kampuni ya Star Infrastructure Limited ambapo hali hiyo imetajwa kuwa inahatarisha hali ya usalama katika eneo hilo.
Watu hao wanaoshikiliwa ni wanaume tisa na wanawake watatu ambao wamekutwa eneo la shamba la mwekezaji lenye ukubwa wa ekari 10,661 wakifanya shughuli za kilimo wakiwa tayari washashafanya uharibifu mkubwa wa mali za mwekezaji.
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Albert Msando amesema kuwa hali hiyo ya sasa ni kukiukwa kwa maagizo ya serikali ambayo yalitolewa na mkuu wa Mkoa na watu 319 walionekana wakiishi eneo hilo la mwekezaji na wakaandikishwa ili waweze kufanyiwa uhakiki na wapewe viwanja lakini wakati wa uhakiki walibainika 169 tu.
“Leo watu waliopo kwenye eneo la mwekezaji ni 767 tukasema haiwezekani tangu miaka mitatu huko nyuma mmekuwa mkiandika barua kuwa mpo 319 lakini ghafla mmefika 767” alisema mkuu wa wilaya ya Morogoro Albert Msando.
Pia ameongeza kuwa watu hao wanaendelea na shughuli zao za kilimo ambapo wanaharibu mali kama kuchoma  mikonge ya mwekezaji ili waweze kulima mazao yao bila kujali gharama zilizotumika na mwekezaji huyo katika kupanda mkonge na hali hii ikitajwa kuhatarisha usalama wa eneo hilo baina ya wakazi na mwekezaji “Nataka tufike mahali tuachane na biashara ya kusumbua serikali kwenda na kurudi kwenye migogoro ambayo haimaliziki”
Licha ya mwekezaji huyo kutoa ekari 4,500 kwa wananchi hao bado wananchi hao wanakimbilia eneo lilitengwa kwa ajili ya mwekezaji huyo hali hii inahatarisha hali ya uwekezaji ilhali kuna madai ya kuwa kuna uwekezaji mkubwa unaotarajiwa kufanyika katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa Afisa mipango miji manispaa ya Morogoro Bi. Emiline Kihunrwa anasema mwekezaji huyo anamiliki eneo hilo tangu mwaka 1953 huku waliovamia eneo hilo wakitajwa kuingia mwaka 2017 na waliandika barua kwenda kwa mkuu wa mkoa, wilaya na kwa mkurugenzi wa manispaa na barua hizo zikionesha watu 319.
“Tulikaa nao kwenye kikao tulikubaliana tukiwa na msimamizi wa shamba hilo na waliomba walime msimamizi aliwaambia kama mnataka kulima kuna taratibu na kama kweli mnataka njooni ofisini tuzungumze lakini hakuna aliyekuja, sisi tulimwambia msimamizi wa shamba kuwa hata kama unamiliki shamba ni jukumu lako kusimamia na kuhakikisha kwamba hawavamii eneo la shamba” Amesema Bi. Emiline Kihunrwa.
Pia Bi. Emiline amesema kuwa wananchi hao wamekuwa wakitoa taarifa za uongo kuhusu eneo hilo, anataja kuwa watumishi wa shamba hilo waliwahi kupeleka idadi ya watu 225, kamati iliyoundwa na mkuu wa wilaya ilibaini kuwepo kwa watu 99 tu (mwaka wa jana 2022) kati ya 225, na hao watumishi wa shamba hilo tuliwaweka kwenye mpango wa kuwagawia viwanja na mpaka sasa hatuna mgogoro wowote.
Licha ya hayo Bi. Emiline amesema kuwa hali hiyo ya sasa ni uvamizi “Mi nadhani ifike mahali serikali ijue kutofautishe siasa za Morogoro na hali halisi, tunawapoteza wawekezaji Morogoro maana kila anapoenda kugusa eneo kinachotokea ni hiki, mtu anafika anajenga kibanda anaanza kulima anasema mmenkuta nalima, amepewa na nani hapa? hakuna ardhi ambayo anapewa mtu bure! kwa hiyo tufike mahali tuchukue hatua zinazotakiwa pia naombeni Serikali mnisaidie, Morogoro ni pagumu kwenye suala la ardhi, tusaidiane” Aliongea kwa uchungu sana.
Ni ukweli usiopingika mkoa wa Morogoro unakabiliwa na changamoto kubwa hasa migogoro ya ardhi, migogoro ya wakulima na wafugaji, na yote hii inatokana na kukosekana kwa maeneo rasmi kwa ajili ya shughuli za kibinadamu.
Watu wengi wanaovamia maeneo ya wawekezaji au maeneo ya hifadhi wanasukumwa na hali mbaya ya kiuzalishaji kwenye maeneo yaliyozoeleka pia hali ya kukua kwa miji kunapelekea wakulima au wafugaji kuhamia maeneo mengine ili waweze kupata malisho na ardhi yenye rutuba.
Njia rafiki ya kufanya ili wananchi wasivamie maeneo ya wawekezaji au maeneo ya hifadhi ni serikali sasa kutenga maeneo ya wakulima, wafugaji na maeneo ya makazi bila ubaguzi na wamna yoyote, pia kuanzisha mashamba ya malisho ambayo wakulima watashirikiana na wafugaji malisho hayo yatawasaidia wafugaji msimu wa kiangazi kupata malisho hii itasaidia wafugaji kutokimbilia maeneo yenye vyanzo vya maji.Mkuu wa wilaya ya Morogoro Albert Msando akitazama kwa makini zoezi la uvunjaji wa nyumba za makazi zilizojengwa na wavamizi eneo la shamba la Mwekezaji.Picha ikionesha baadhi ya mikonge ambayo imeshaharibiwa na wananchi kwenye eneo la mwekezaji.Picha ikionesha Migambo wakiwa wanavunja nyumba mojawapo ambayo imejengwa na wavamizi eneo la kwenye shamba la mwekezaji Manispaa ya Morogoro.
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Albert Msando akiwa ameshika mkonge ambao umeshakatwa na wavamizi kwenye shamba la mwekezajiMwisho.
Twitter
0
Copy
0
Facebook
0
Recent Comments