Recent Comments

WAZAZI WASHAURIWA KUWATHAMINI WATOTO WAO, KUJENGA KIZAZI BORA.

By Mussa Mathias Aug 25, 2024
Picha: Askari polisi akifurahi na watoto.

WAZAZI WASHAURIWA KUWATHAMINI WATOTO WAO, KUJENGA KIZAZI BORA.

Morogoro.

Uwepo wa ongezeko la mmonyoko wa maadili vitendo vya ukatili pamoja na unyanyasaji kwa watoto umetajwa kusababishwa na baadhi ya wazazi kushindwa Kuishi na watoto ba badala yake kuwaachia wasichana wa kazi Hali ambayo imesababisha watoto wengi kukosa Malezi yaliyo Bora

Katika hiyo ameelezwa kuwa hali kwa sasa siyo salama kwani watoto wengi wanafanyiwa vitendo vya ukatili, unyanyasaji na kukosa sehemu ya kwenda kutoa taarifa kwani wazazi wengi hawana muda wa kuwasikiliza watoto wao.

Akizungumza katika kuhitimisha mashindano ya mtoto bomba Diwani wa Kata ya mji mpya Manspaa ya Morogoro amesema kuwa ipo haja ya kuandaa makongamano mbalimbali yatakayoweza kuwakutanisha watoto na kuwapa elimu juu ya ukatili unaofanywa na kusababisha kuharibika kwa kizazi Bora

Kwa Upande wake Paschal Elias mkurugenzi wa mashindano ya mtoto bomba amesema kuwa kwa kutambua jitihada zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Dk. Samia Suluhu Hasani wameunga Mkono kwa kuanzisha mashindano haya yenye lengo la kuinua vipaji pamoja na kutoa elimu kwa watoto dhidi ya ukatili

Hata hivyo ameziomba Serikali pamoja na wadau mbalimbali kushirikiana katika mashindano haya ikiwa lengo kuu ni kupunguza na kumaliza ukatili kwa watoto pamoja na kuandaa na kutengeneza kizazi kilicho Bora

Naye Koplo wa polisi (CPL) Suleiman Ibrahim Kova wa Dawati la Jinsia amewataka wazazi kukaa na watoto wao na kuacha kuwategemea walimu wao kwa asilimia kubwa kwani mtoto ana nafasi kubwa ya kumweleza mzazi wake juu ya mambo mabaya anayofanyiwa

Mashindano ya mtoto bomba yalianza tangu julai 1 na kutamatika agosti 24 huku shule mbalimbali kutoka Mkoani Morogoro zikishiriki na yanatarajia kufanyika tena Disemba 2024 yakiambatana na matukio mbalimbali kama kwenda kutoa msaada katika vituo vya watoto yatima mkoani Morogoro.

Mwisho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *