WAZIRI MCHENGERWA AZINDUA MAGARI 22 YA DORIA TAWA, AHIMIZA KUCHAPA KAZI
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb) leo Februari 16, 2023 amezindua magari 22 ya TAWA yatakayotumika Kwa ajili ya shughuli za doria na kudhibiti Wanyamapori Wakali na Waharibifu.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa magari hayo iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya TAWA Mkoani Morogoro Mhe. Mchengerwa ameushukuru uongozi wa TAWA Kwa kutenga fedha ambazo zimewezesha kununua magari hayo ambayo yatatumika katika shughuli za doria, kudhibiti ujangili na Wanyamapori Wakali na Waharibifu.
Waziri Mchengerwa amesema mbali na shughuli za kudhibiti ujangili, magari hayo yatumike pia katika kujenga mahusiano mazuri na Wananchi wanaozunguka maeneo ya hifadhi.
Mhe. Mchengerwa ameagiza watumishi wa Wizara yake kujipanga katika kuhifadhi rasilimali za Nchi hii, kuongeza Kasi ya kutangaza Vivutio vya Utalii vilivyopo Nchini na kufanya kazi Kwa bidii.
“…Tujipange kwenda kuhifadhi sana, tuhifadhi kwelikweli, zile changamoto tunazoweza kuzitatua ni Lazima tuzitatue” amesema
“Nitataka Kila mmoja wetu akafanye kazi kwenye eneo lake, na afanye kazi kwelikweli, kama utatakiwa kuwepo kwenye eneo lako Saa sita mchana uwepo kwenye eneo lako” amesisitiza Waziri Mchengerwa.
Ameongeza kusema pamoja na kazi nzuri za kuhifadhi zinazofanywa na TAWA na Taasisi zingine za Uhifadhi bado asilimia 21 ya pato la Taifa linalochangiwa na Wizara ya Maliasili ni dogo kulinganishwa na wingi wa rasilimali zilizopo katika Taifa hili, hivyo amehimiza kuongeza kasi ya kutangaza vivutio vya Utalii Ili kuongeza pato la Taifa.
Hii ni ziara ya kwanza ya Mhe. Waziri Mchengerwa tangu kuteuliwa kwake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii ambapo aliongoza na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbas Said ambaye nae aliteuliwa hivi Karibuni.
Wengine waliongozana na Waziri Mchengerwa ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Juma Mkomi,
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bi Prisca Lwangili na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori , Dkt. Maurus
Recent Comments