Habari zinazosambaa hivi sasa zinaeleza kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima ameliagiza Jeshi la Polisi pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini ( Takukuru) kumkamata na kumhoji mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu
Dk Gwajima ametoa agizo hilo leo Jumanne Agosti 17, 2021 akiwa Wilayani Butiama  akieleza kuwa  Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi jambo linaloivuruga  wizara yake na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo
Inafahamika kuwa, Askofu Gwajima amekuwa akisisitiza kuwa hatakubali kupatiwa chanjo ya kukabiliana na Uviko-19
Licha ya kuwa Gwajima ni Mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Kiongozi mkuwa amekuwa akitoa kalu za kupingana na Chanjo inayotangazwa na Serikali, ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwataka wabunge kujitokeza kuchanja na kwamba japo ni hiyari lakini hakuna hiyari ya kuwaambukiza wengine Uviko-19.
Recent Comments