Msimamizi wa zahanati ya kijiji cha Kabanga kata ya Kabanga iliyopo wiayani Ngara mkoani Kagera ametoa ufafanuzi juu ya habari iliyo tolewa na simamia.com kuhusiana na mama mjamzito alie fika katika kituo hicho siku ya Desemba 12,202 kwa kusema kuwa mgonjwa huyo alipatiwa matibabu isipokua ndugu na jamaa wa mgonjwa huyo walitoa maelezo ambayo hayakua ya kitaalam.
Aidha msimamizi huyo amesema kuwa mjamzito huyo alimpokea yeye mwenyewe majira ya saa4 za asubuhi na kumpatia sindano moja ya asubuhi ambapo alipaswa kuchomwa nyingine majira ya saa 4 za usiku lakini ndugu wakashindwa kuvumilia wakaomba msaada kwa simamia.com kumfikisha kituo cha afya cha mabawe ambapo tayari alikua amekwisha kuchomwa sindano yapili.
Vilevile msimsmizi huyo amesema kuwa inaonesha ndugu wa mgonjwa huyo apatiwe dripu na hali kua hali ya mgonjwa huyo hakustahili kuwekewa dripu kwani alimpatia dawa ya kumuongezea nguvu baada ya mgonjwa kulalamika anahisi maumivu ya tumbo.
Pia simamia.com imemuuliza kuhusiana na malalamiko ya baadhi ya wananchi wanao lalamikia kufanyiwa vitendo vya kuashiria kuombwa huduma ya mapenzi amesema suala hilo kwa upande wake halifahamu lakini ameiahidi simamia.com kuwa anaenda kulifanyia kazi na endapo litabainika lipo katika zahanati hiyo wahusika watachukuliwa hatua.
Hata hivyo msimamizi huyo amewataka wanachi kuendelea kupata huduma katika kituo hicho kwani ni sehemu salama kwao na kuwataka kumpa taarifa endapo watafanyiwa vitendo visivyo faa pamoja na kuweka maoni kwenye sanduku la maoni kwaajili ya kuimalisha huduma za zahanati hiyo.
Lakini pia simamia.com imeendelea kufuatilia taarifa za mgonjwa mpaka kufikia jioni ya Decemba 13, 2023 mgonjwa bado amelazwa kaika kituo cha afya cha Mabawe huku hali yake ikiendelea kuimarika.
Recent Comments