NA MWANDISHI WETU
Siku ya Desemba 12,2023 imekua siku mbaya na ambayo haitasahaulika maishani mwa mama mjamzito mkazi wa kitongoji cha Kumshiha kijiji cha Kabanga ambaye jila lake limefadhiwa baaada ya kufika katika zahanati ya Kabanga,kijiji cha Kabanga, kata ya Kabanga iliyopo wilayani Ngara mkoani Kagera.
Ilikua majira ya asubuhi mara baada ya mama huyo kujihisi afya yake kutokua nzuri alifika katika zahanati hiyo kwaajili ya kupata matibabu, baada ya kufika zahanati alipimwa na kugundulika kuwa ana ugonjwa wa maralia na UTI lakini hakupata matibabu mchana kutwa licha ya kuendelea kutapika na kukosa nguvu mwilini hali iliyo pelekea aendelee kulala katika zahanati hiyo.
Hata hivyo ilipofika majira ya jioni majirani wa karibu waifika katika zahanati hiyokwa lengo la kumjulia hali mgonjwa lakini walipofika katika zahati hiyo wakakuta bado hali ya mgonjwa inazidi kuwa mbaya jambo ambalo liliwafanya wamuite daktari ndipo daktari huyo alikuja akiwa amevalia Kaushi alimaarufu kama Singrendi, Katika hali isiyo ya kawaida daktari huyo alievalia kaushi alimshika jirani mmojawapo na kuvutia nje ya chumba alichokua amelala mgonjwa kwa madai anataka kumpa maelekezo ya matumizi ya dawa anazo takiwa kupewa mjamzito huyo.Kutokana na hali hiyo jirani alitiwa hofu na mvutano usio wa kawaida kutoka kwa daktari hiyo na kujiuliza kwanini asinge pewa maelekezo hayo mbele ya mjamzito huyo na ikizingatiwa ni majira ya saa mbili za usiku na jirani huyo ni wa njinsia ya kikke na daktari akiwa ni jinsia ya kiume.
Vilevile baada ya jirani kuonesha mashaka na kuto kutoa ushirikiano kwa yale aliyo yataka daktari huyo alikasirika na kusema kama amekataa basi haina haja ya kumpatia tena maelekezo ya dawa hizo maaana hazifai tena, Ndipo jirani huyo ambae jina lake ameiomba simamia.com isilitaje akaamua kumuita ndugu wa karibu wa mja mzito huyo.Ndugu wa karibu ambae pia jina lake limehifadhiwa alipo fika zahanati nakuona hali ya mama mjamzito ikazidi kuwa mbaya aliamua kumpigia daktari ambae alimjibu kuwa hayupo kazini yupo likozo akamuahidi kuwasiliana na mhudumu aliepo karibu.
Baada ya muda mchache mhudumu huyo alievalia kaushi huku akijiongelesha na kujichekesha alisema ngoja amchome sindano kasha akamchoma sindano mbili ambazo simamia.com haikubahatika kubaini zilikua dawa gani na za ugonjwa gani?
Ilipo fika saa3 za usiku simamia.com ilipokea simu kutoka kwa ndugu wa karibu ili tuweze kufika katika zahati hiyo kushuhudia kinacho endelea ndipo jirani mmojawapo alisema “Ni bora waje hao simamia.com watusaidie” muuguzi huyo ndipo aliogopa na kutaka kumwekea mgonjwa dripu ya maji, lakini katika hali isiyo ya kawaida baada ya kusikia muungurumo wa gari alitimua mbio huku akiwa na kaushi yake na kuamua kujifungia ndani na kufungulia muziki mnene.
Pia simamia.com baada ya kukosa ushirikiano na daktari huyo iliamua kuwasha gari na kumchukua mjamzito huyo na kumkimbiza katika kituo cha afya cha Mabawe kwani hali yake ilikua ni mbaya na yakutisha ikizingatiwa anakiumbe tumboni.
Baada ya kufika kituo cha afya Mabawe Daktari wa zamu alihitaji maelezo kutoka zahanati ya Kabanga ikiwemo vipimo na dawa alizo tumia lakini hazikuwepo kutokana na daktari wa zahanati kutoonyesha ushirikiano, Ndipo ubinadamu na utu wa daktari wa zamu katika kituo cha afya Mabawe alimpoke mama huyo majira ya saa 5 za usiku na kasha kumfanyia vipimo upya na kugundulika kuwa ana ugojwa wa Maralia na UTI lakini akashindwa kumpa dawa kwasababu hakujua ni sindano gani alizochomwa mama huyo.
Mpaka simamia.com inaondoka katika viwanja vya kituo cha afya Mabawe majira ya saa 6 za usiku mgonjwa alikua amelazwa na kuwekewa dripu ya maji huku akisubiria kukuche ili mgonjwa huyo aweze kuanzishiwa dozi ya Maralia na UTI.
Lakini pia simamia.com haijaishia hapo imefika katika kijiji cha Kabanga na Mrukukumbo na kuzungumza na baadhi ya kina mama ambao wameiomba simamia.com kuficha majina yao ndipo tukaamua kuwabatiza majina kama Mama Jaye huyu ni mkazi wa mrukukumbo yeye anasimulia kuwa kuna siku aifika katika zahanti hiyo akiwa ana maumivu ya tumbo lakini badala ya kupewa huduma alicheleweshwa na kutomaswa jambo lilimfanya aichukie zahanti ya kabanga mpaka hivi sasa akiugua anaenda vituo vya watu binafsi kwa kuogopa kudharirishwa’ Mkazi wa kijiji cha Kabanga tumembatiza Madame E nayeye anasema mara kadhaa akienda zahanati hapo kunadaktari mmoja wapo amekua akimuonesha kutaka kumpa huduma ya mapenzi badala ya kumpa huduma ya matibabu jambo lililomfanya kwasasa aogope kwenda zahanati hiyo pale anapo ugua.
Kazi ya simamia.com ni kuonesha lakini kazi ya kuchunguza jambo hilo ni jukumu la wahusika yapo mengi hayajaandikwa humu na yanatendeka lakini simamia.com tunaamini tumetoa mwanga wa kubaini na mengine yanayo fanana na haya.
Recent Comments