Taarifa zinaonyesha wanaume wengi hujikuta wakinasa na kununua vifaa hivi kwa sababu ya kuathirika kwao kisaikolojia ambako huongeza shauku iliyopitiliza ya kuongeza maumbile mkubwa Ambayo huweza kuwasababishia maumivu wenza wao, jambo litakalofanya mwisho wa siku wasifurahie tendo hilo na kuongeza uwezekano wa kupata hofu kutokana na ukubwa huo.
Wasichokijua ni kwamba kinachotakiwa ni kuwa na uume wa wastani kuliko mkubwa uliopitiliza unaoweza kuwasababishia maumivu wenza wao, jambo litakalofanya mwisho wa siku wasifurahie tendo hilo na kuongeza uwezekano wa kupata hofu kutokana na ukubwa huo.
Kuna moja ya kitabu cha simulizi kilikuwa kikielezea namna ya kujiondoa kwenye aibu ya kuwa na uume mkubwa huku kikimtaja Napoleon Bornaparte kuwauwa wajakazi wake walipomcheka uume mkubwa na kutaja pia watu waliokuwa na uume mkubwa akiwemo Abrahan Lincoln, Esteern, na wengine wengi ambayo hii inaonesha kiasi gani kipindi cha nyuma ilikua ni kero lakini sasa ndiyo imekuwa mada na kuwafanya wanaume kuathirika kisaikolojia na kufanya namna kuongeza.
Laiti kungelikuwa na njia salama za kunenepesha na kurefusha maumbile katika huduma rasmi za afya, gharama za kuchangia matibabu zingekua maradufu. Kwa sababu wanaume wengi wanaodhani wana maumbile madogo ya uume wangemiminika kwenda kutibiwa tatizo hilo.
Licha ya hilo pia Mamlaka za ndani na kimataifa kama vile Wizara ya Afya, Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Shirika la Afya Duniani (WHO) na vyuo vikuu vilivyobobea kufanya utafiti kikiwamo Havard, hakuna mahala ambapo wamepitisha na kupendekeza dawa au kifaatiba kwa ajili ya huduma hiyo.
Watu wanene kupitiliza, shina la uume lililo chini ya kitovu humezwa na mafuta na nyama zilizorundikana hapo, hivyo kupunguza urefu wa kiungo hicho muhimu kwa tendo la ndoa.
Zipo njia chache ambazo jumuiya za kimataifa na mamlaka za afya wanakubali kuwa zinaweza kusaidia angalau kuongeza urefu, lakini usiozidi nchi moja, njia hizo ni pamoja na kupunguza unene.
Japo njia ya upasuaji nayo sio nzuri sana, maana haiendi kuondoa chanzo…njia nzuri ni ile ya kubadili mtindo wa maisha kwa namna nzuri, ya ulaji, mazoezi na kunywa maji ya kutosha…ambayo itaruhusu mwili kupungua vizuri bila kusumbuliwa.
Hivyo, kupunguza unene kwa njia ya vyakula na mazoezi inakubalika. Vilevile kwa njia ya upasuaji kwa lengo la kupunguza mafuta ya eneo hilo inakubalika pia.
Vitu vinavyotumika kiholela kunenepesha na kurefusha uume ni pamoja na vidonge, sindano, virutubisho, mashine maalumu, upasuaji wa kupandikiza, vifaa vya mazoezi ya uume, mafuta ya kupaka uumeni na mitishamba.
Vitu hivi vinauzwa kisiri katika baadhi ya maduka ya dawa, kwa njia ya mtandao, kutembezwa mtaani au matangazo kwenye magazeti na vyombo vingine vya habari.
Lakini, kati ya hivyo nilivyotaja, hakuna vinavyofanya kazi kwa ufanisi na kukidhi vigezo vya kitaalam kupitia vyombo vikubwa vya matibabu na uthibiti wa magonjwa ikiwamo WHO.
Kwa sababu hakuna utafiti wa kisayansi kuthibitisha ubora, ufanisi na usalama wa vifaatiba hivyo au njia zilizopendekezwa ingawa ni kweli, vipo baadhi ambavyo kwa muda mfupi, vinaweza kukusaidia lakini vikikuacha na madhara makubwa hapo baadaye.
Madhara hayo ni pamoja na kupungua au kukosa kabisa nguvu za kiume, kuchubuka uumeni, kuvunjika kwa misuli sponji ya uume, madhara ya nerve na kupata maumivu sugu wakati wa kujamiana.
Mwanaume tambua tu kuwa mazoezi ni lazima na muhimu sana usijidanganye fanya zoezi tu pia usisahau kutafuta na kutunza hela.
Recent Comments