Watu wengi huujua mchaichai kama majani ambayo yanaweza tumika kuandaa chai pia kutumika kama dawa ya Mbu bila kutambua kuwa mchaichai una faida nyingi za kiafya, Mchaichai hutajwa kuwa ni kinywaji chenye uwezo wa kupunguza joto unapotumia chai yake husaidia kuondosha joto kwa mtu mwenye homa.
Licha ya hayo mchachai una faida nyingi zaidi ambazo ni kama vile
Hukinga mtu dhidi ya Saratani au Kansa, Moja ya Tafiti ya wanachuo wa Gurion nchini Israel waligundua kwamba majani haya huua seli zinazopelekea Saratani hivyo basi kumkinga mtu asiipate.
Husaidia katika mmeng’enyo wa chakula mtu anapotumia kinywaji cha mchaichai hasa chai yake husaidia suala la umeng’enyaji wa chakula ambapo pia hutibu suala la kuhara au tumbo kujaa gesi na maumivu yake.
Pia majani haya husafisha figo ambapo figo hiyo husaidia kuchuja damu na kuondosha mafuta hatari katika mwili ambayo huweza pelekea magonjwa hali inayo imarisha afya zetu.
Huzuia maumivu wakati wa hedhi, wanawake wengi hukumbana na maumivu makali wanapokuwa na hedhi hasa tumbo wengi wao huita chango hivyo basi unapotumia majani hayq husafisha mirija na kurahisisha damu ipite bila kusababisa maumivu.
Husafisha damu na kuepusha kuugua majipu ambapo husaidia wale wanaoathirika na magonjwa ya ngozi hivyo basi ni vyema kuutumia mara kwa mara.
Pia humsaidia mama mjazito kujifungua kwa njia ya kawaida ambapo hulegeza nyonga na kufanya mtoto kutoka kiuarahisi hivyo atumie mara kwa mara.
Humpunguzia mtu mwenye vidonda vya tumbo kwa kuondoa gesi inayokuwa tumboni na kupelekea maumivu.
Pia hupandisha CD4 Kwa wagonjwa wa ukimwi, ambapo inashauriwa mgonjwa atumie mara kwa mara mchaichai kuliko majani ya chai ili kuimarisha afya yake.
Recent Comments