Mtoto akiwa mdogo huhitajika kupata lishe iliyo bora kwakuwa ndiyo wakati ambao mwili na afya ndiyo hujengeka hivyo ni muhimu kuandaliwa chakula chenye virutubisho vyote na muhimu.Chakula hicho cha mtoto ni rahisi kutengenezwa ila msingi sana huhitaji usafi wakati wa kuandaa.
Ili kulinda afya ya mtoto, andaa vyakula kama ifuatavyo
i) Mboga mboga pamoja na matunda hii husaidia kumuongezea vitamini anza kwa ku osha mboga zako kwa maji safi na yenye uvugu vugu kisha ikatekate injika halafu weka kichumvi kidogo sana ila mafuta usiweke subiri mboga Ikichemka saga mboga hiyo kwa blender au ponda ponda ndiyo mpe mtoto ikiwa laini, na matunda yaoshe vizuri afu kata vipande vikubwa ili mtoto asije jikaba au pondaponda ndo umpe mtoto kumbuka kuto ganda nje.
ii) Samaki na Nyama, katakata nyama vipande vidogovidgo chemsha mpaka ilainike kabisa kisha isage kwenye food machine mpe mtoto na supu yake kwa upande wa samaki si lazima kusaga mana ni laiini ikiiva tu ila hakikisha unatoa mifupa yote mana ni hatari kwa mtoto.
iii) Vyakula vya mbegu kama vile maharage, kunde, njegere hivi jumpa protini hivyo vichemshwe mpaka vilainike kabisa pondaponda ndipo umpe pia ndizi na viazi vinafaa ukichanganya na mchuzi wa nyama au samaki hufaa sana kwa watoto.
iv) Vyakula vya Nafaka, watu wengi hupenda changanya nafaka mbalimbali kwenye unga wa uji wa mtoto lakini siyo vizurisana kuchanganyachanganya nafaka kwenye uji wa mtoto ila unaza ongeza unga wa karanga unapopika uji ili kuongeza fati kwa mtoto.
Ili kuhakikisha usalama wa mtoto wako, Fanya haya wakati wa kula.
1: Usimwache mtoto ale mwenyewe wala anywe akiwa peke yake mana anaweza jikaba au kuoaliwa yakatokea mengine.
2: Epusha kumpa chakula kinachoeza mkaba au mpalia mtoto mfano punjepunje kam vile karanga, mahindi pia zabibu.
3: Hakikisha joto la chakula ni rafiki kwa mtoto kabla ya kumpa ili kuepusha kumuunguza. .
4: Muhimu kuwepo na usafi ili kulinda afya ya mtoto.
Recent Comments