Mama anapokuwa mjamzito huwa tofauti kifogo na wakati akiwa kawaida kwa kuwa huwa yeye pamoja na kiumbe kingine hivyo basi huhitaji lishe bora ambayo itakuwa na matokeo chanya kwa afya yake na kiumbe kilichopo tumboni mwake ambapo kinatakiwa kiwe kina virutubisho vya kutosha ili kuimarisha afya ya mhusika.
Kiukweli mama mjamzito anapokosa lishe bora hupeleka matatizo kwa mama mwenyewe na hata mtoto ambapo huweza pelekea mtoto kufia tumboni, kuzaliwa kabla ya wakati, mama kupungukiwa damu na mengineyo ambayo ni hatari.
Mama mjamzito unatakiwa kulinda afya yake ambapo unahitajika kupata lishe iliyo bora na ya kutosha kama ifuatavyo;
A) Tumia milo hadi minne kwa siku moja pia kula vitafunwa kila mara kadri iwezekanavyo ili mwili upate nguvu pia lishe ya mtoto tumboni vitafunwa huweza kuwa karanga, mahindi mchemsho auya kuchemshwa, yai, maziwa na vinginevyo.
B) Usipendelee kutumia chai wala Kahawa unapokula kwasababu huweza ingilia ufyonzwaji wa virutubisho mwilini.
C) Meza vidonge vinavyoongeza damu yaani FEFO kipindi chote cha ujauzito wako kila siku usiache kabisa.
C) Ili kuongeza damu kwa haraka pendelea vyakula vya nyama yaani kuku, nyama, samaki na vinginevyo.
D) Tumia matunda mbalimbali vya kutosha na mboga mboga aina mbali mbali kwa wingi.
E) Wakati wote wa ujauzito tumia chumvi iliyo na madini joto.
F) Hakikisha unakunywa maji kwa wingi walau glasi 8 hadi lita 1. 5.
G) Jikinge na Malaria kwa kuwa na chandarua pia tumia dawa za kuzuia malaria, minyoo kwaajili ya afya ya mtoto tumboni.
Kumbuka: Utumizi wa sigara au pombe maana ni hatarishi kwa afya ya mama na mtoto.
@Ventas Malack
Recent Comments