NA, MWANDISHI WETU.
Ngara ni wilaya mojawapo katika mkoa wa Kagera ikiwa ni wilaya yenye fursa nyingi zinazo weza kuifanya Ngara kuwa tajiri lazkini zaidi inazidi kuonekana kuwa ni wilaya masikini ukilinganisha na rasilimali zilizopo.
Ni aibu kubwa katika wilaya kubwa kama Ngara na yenye wasomi wanao shinda wanasifiana Wasifi wao (CV) zao na rasilimali nyingi zinazo weza kuingiza pesa viongozi wakifurahia mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF ukishamiri na watu wakiendelea kuwa masikini.
Aidha wakulima waliahidiwa kupewa miche kadhaa ya parachichi lakini mpaka sasa licha ya serikali kuombwa fedha nyingi kwaajili ya kupata miche hiyo bado ni miche itakayo elekezwa kwa wakulima wenye uwezo badala ya kuelekeza miche hiyo katika kaya zinazo tajwa kuwa ni masikini zinazo tegemea misada kila kukicha na zinazo ishi kwa kutegemea misada na kufanyishwa vibarua vya kutoboa barabara mpya za mitaa kwa kutumia majembe ya mkono na kuambulia Tsh 3,000 kila wanapo pewa kazi hiyo.
Ifahamike kuwa familia nyingi ambazo asili yake ni wilayani Ngara zinamiliki vipande vya aridhi vyenye uwezo wa kubeba miche ya parachichi isiyo pungua mitano ambayo kwa wastani katika kila msimu baada ya kuanza kuvuna zinakua na uwezo kuvuna parachichi zenye thamani isiyo pungua Tsh Millioni 1.5 na kuendelea fedha zinazo tosha kufuta sifa ya kuitwa kaya masikini badala ya kuendelea kuishi kwa kutegemea misaada kama ilivyo hivi sasa.
Kama serikali inavyo fuatilia na kisajili watu wanao tambulika kama kaya masikini ipo haja ya serikali kuweka mpango wa kugawa miche ya parachichi katika kila kaya masikini na kufatilia upandaji na uhudumiaji wa miche hiyo kama wanavyo wafatilia kuwapelekea misaada na kuwalimisha kwneye kutengeneza barabara mpya za mitaa kwa malipo ya Tsh3,000 kila wanapo hitajika kufanya kazi hizo.
Hata hivyo Ngara kama wilaya yenye bahati ya kuwa na mipaka mikuu miwili Rusumo kuihudumia Rwanda na Kabanga Kuihudumia Burundi pamoja na Murusagamba mpaka unao hudumia pia Burundi, kuna haja ya serikali kuweka miundo mbinu mizuri ya kibiashara ili watu kutoka nchi jirani wawe wanapata bidhaa nyingi karibu badala ya kufuata bidhaa hizo Shinyanga,Mwanza na Dar es salaam jambo linalo weza kuongeza mapato na fursa za ajira kwa wakazi wa Ngara na hata asilimia ya mapato ya ndani kwaajili ya kufanya maendeleo ya Ngara.
Viongozi wanapaswa kutambua kuwa Ngara bila kuwa na kaya masikini ni kitu ambacho kinawezekana ni suala la viongozi kuona umuhimu wa hilo na kuchukua hatua za dhati kwakua kufuta kaya masikini ndani ya miaka mitano ni jambo ambalo linawezekana.
Recent Comments