NGARA HAKUNA USHINDANI WA VYAMA VYA SIASA VYA UPINZANI ILA KUNA USHINANI NDANI YA CCM

By Simamia Ngara Mar 17, 2024

NA, ANKO G.

Wilaya ya Ngara/Jimbo la Ngara linalo patikana Mkoa wa Kagera ni Wilaya/Jimbo ambalo halina ushindani wa vyama vya siasa vya upinzani na hili linaweza chukua hata zaidi ya miaka 20 ijayo bila kuwa na ushindani wa vyama vya siasa vya upinzani dhidi ya chama tawala Cahama Cha Mapinduzi (CCM).

Aidha wilaya ya Ngara/Jimbo la Ngara lina upinzani/ushindani ndani cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) hii ni kutokana na walio chaguliwa katika nafasi mbalimbali hasa Ubunge na Udiwani kuonesha hofu ya kuondolewa katika nafasi zao hata kabla ya muda wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Imekua kawaida kushuhudia baadhi ya viongozi wa chama hicho wakiwahofia wanachama wenzao kuwa huenda wanaweza kugombea nafasi hizo na pengine kudhani kuwa wanaweza wasirudishwe katika nafasi hizo licha ya kuamini kazi wanazo fanya tangu kuchaguliwa na hivyo kutumia nguvu na mbinu nyingi kilinda nafasi zao ili waweze kuchaguliwa tena mwaka 2025 wa kile wanacho kiita kuongezewa mitano tena.

Hata hivyo viongozi hao hawana hofu ya wagombea kutoka nje ya chama hicho bali hofu yao ni wagombea wanao tokana na chama hicho na wamekua wakinukuliwa katika mikutuno yao ya hadhara wakionesha hofu ya wanachama wenzao wanao hisi kuwa huenda watagombea nafasi hizo na wengi wao wakitajwa kuwa ni wazee wastafu.

Lakini pia Jimbo la Ngara siyo miliki ya mtu mmoja wala chama kimoja bali kila mtu anahaki ya kutangaza, kuomba nafasi ya kuchaguliwa kwanafasi yoyote ile,kutangaza sera zake na bila kujali chama chake,umri,kabila wala dini yake na mengine yanayo fanana na hayo ilimradi awe na sifa zilizo ainiahwa katika katiba ya nchi na miongozo ya uchaguzi unao tokana na vyama vya siasa, swali wanalo jiiliza watu wengi ni kwamba kwanini wenye nafasi hizo hawana imani kuwa wataongezwa mitano tena?

Pia ninapo zungumzia kuwa Ngara inaweza kukosa ushindani wa vyama vya upinzani hata kwa zaidi ya miaka 20 hii ni baada ya vyama vya siasa vya upinzani kukosa mvuto na kutotangaza sera kwa wanachi kama ilivyo katika majimbo jirani kama vile Biharamulo,Muleba na Bukoba kwasababu vyama vya upinzani Ngara havionekani kufanya mikutano ya hadhara, kuonekana wakizungumza kwenye vyombo vya habari wala kuvitangaza vyama vyao na kutafuta wanachama wapya jambo hilo linafanya vyama hivyo kupoteza mvuto kwa wanachi na hata kuto ona umuhimu wa vyama hivyo katika wilaya na Jimbo lao.

Vyama vya upinzani Ngara vinapaswa kujifunza kutoka kwa majimbo jirani ambapo vyama vya upinzani vimekua karibu na wanachi, kutetea na kupambania wanachi pale vyama hivyo vinapo ona inafaa kufanya hivyo.

Hata hivyo vyama hivyo vya upinzani Ngara havijawekeza kwa vijana kwa sana kama ilivyo kwa chama tawala jambo linalo pelekea vyama hivyo kukosa nguvu na kuendelea kukosa nguvu zaidi kadri miaka inavyo sogea kwasababu vijana ndio wenye nguvu na uwezo wa kushawishi watu kujiunga na vyama hivyo.

Jamii itambue kuwa upinzani ni kichocheo cha maendeleo kwasababu wenye nafasi hulazimika kufanya kazi kwa bidii kwakuhofia kiwa wasipo fanya kazi nzuri wanaweza kuondolewa katika nafasi zao hivyo upinzani na vyama vya upinzani ni kichochoe cha maendeleo katika jamii na ndiyo maana majimbo yenye upinzani yanakua na maendeleo.

One thought on “NGARA HAKUNA USHINDANI WA VYAMA VYA SIASA VYA UPINZANI ILA KUNA USHINANI NDANI YA CCM”
  1. Kuwa mpinzani na wewe ulete huo mvuto, sisi tunaamini tumepambana kadri ya uwezo wetu

Comments are closed.