Mwanariadha wa Kenya Ezekiel Kemboi ameshinda medali ya nne mfululizo katika mashindano ya dunia mjini Bejjing baada ya kuwaongoza Wakenya wenzake kushinda nafasi za kwanza nne bora.
Awali mwanariadha wa Kenya Vivian Ceruiyot aliishindia Kenya medali nyingine ya dhahabu na baada ya kushinda mbio za mita 10,000 kwa upande wa wanawake.
Vivian alishinda medali za fedha mbio za mwaka 2003,2005,2007.
Mwanariadha wa Ethiopia Gelete Burka alichukua medali ya fedha baada ya kushindwa kumpita Cheruiyot.
Medali ya shaba ilimwendea Mmarekani Emily Infield ambaye alishinda medali hiyo baada ya kumpita Molly Huddle katika utepe.
Upande wa wanaume katika mbio za kuruka maji na viunzi mita 3000,Conseslus Kipruto alichukua fedha,Brimin Kipruto akachukua shaba huku Jairus Kipchoge Birech akichukua nafasi ya nne
Mpinzani wao raia wa marekani Evan Jagger aliona kivumbi wakati Wakenya hao walipotimka mbio.
Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on.
Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments