VIJANA wengi wamekuwa wakikimbia kilimo vijijini wakidhani kuwa hakina faida yoyote.
Hawafahamu kuwa siku zote mwanzo ni mgumu kwani hata waliofanikiwa awali walikuwa maskini na hawakuwahi kufikiria kama watakuja kuwa matajiri wakubwa duniani.
Kilimo na biashara ni miongoni mwa vitu vilivyochangia utajiri wa watu wengi ndani na nje ya nchi. Hata siku moja huwezi kumiliki mabilioni ya fedha kwa kutegemea kuajiriwa.
Katika makala haya kutana na mfanyabiashara wa kwanza wa Kitanzania
kufanya biashara ya kusafirisha korosho kwenda nchini Vietnam, Abbas Maziku ambaye anaelezea alipoanzia, vikwazo anavyokutana navyo, mafanikio na matarajio yake kibiashara.
Maziku ni kijana wa Kitanzania aliyezaliwa mwaka 1990 mkoani Mwanza.
Kitaaluma ni mtaalamu wa masuala ya kibenki na fedha ambapo alipata Shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Zanzibar.
Baada ya kuhitimu masomo yake aliajiriwa katika Benki ya Exim kama ofisa biashara.
Alidumu na kazi hiyo kwa muda mfupi na kuamua kugeukia biashara ya mazao.
Alipoanzia
Akizungumza na mwandishi wa makala haya, Maziku anasema alipoona kazi ya kuajiriwa haina maslahi, aliamua kuanza biashara ya kusafirisha mazao, hiyo ilikuwa mwaka 2013.
Anasema alijikita katika biashara hiyo baada ya kuvutiwa na mjomba yake aliyekuwa akimiliki mashamba yenye mazao mbalimbali.
Miongoni mwa mazao ambayo Maziku alianza nayo na anendelea nayo mpaka sasa ni korosho, ufuta, mbaazi, choroko, mtama, alizeti, mashudu ya pamba na pilipili manga.
Akizungumzia anapoyapata mazao hayo anasema; âninachofanya nakusanya mazao kutoka kwa wafanyabiashara wadogo wadogo ambao hukusanya mazao kwa wakulima na katika minada inayofanywa na vyama vya ushirika mkoani Lindi, Mtwara, Dodoma, Singida, Shinyanga na Tanga ambayo hufanyika mara moja kwa kila wiki.â
Anasema baada ya hapo husafirisha mazao hayo kutoka mikoani na kwenda kuyahifadhi kwenye magahala yanayotumika kuhifadhi mazao.
âWakati wa kuyafungasha unapofika huwa nawatumia vibarua na katika vifungashio vyangu huwa na nembo inayoonyesha jina la kampuni yangu.
Baada ya hapo sampuli hupelekwa katika maabara za kupima ubora wa mazao kimataifa iitwayo SGS,â anasema na kuongeza:
âMazao haya huwa nayasafirisha kwenda nchini Vietnam kwa kutumia meli za mashirika mbalimbali ikiwamo IPTL, MAERSK na nyinginezo.â
Anabainisha kuwa huwa hatumii njia za panya, hufuata hatua zote zinazohitajika ikiwamo kupata kibali cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wizara ya Kilimo na Ufugaji, wanasheria pamoja na maofisa wa usalama wa taifa ambao uhakikisha hatua zote halali zimefuatwa.
Anasema biashara ya mazao kupeleka nje ya nchi ina ushindani mkubwa hivyo inahitaji umakini mkubwa ili kuweza kujiendeleza, la sivyo unaweza kuishia njiani kwa kupata hasara.
Anasema anakumbuka alianza na mtaji wa Sh milioni mbili na sasa anazungumzia mtaji wa Sh milioni 200.
âSi rahisi kufika nilipofikia, kwa sababu biashara hii ina ushindani mkubwa.
Ninashindana na matajiri wakubwa wenye uwezo wa kujipangia bei za mazao hivyo ingawa nimepiga hatua lakini bado ninahitaji kupanua biashara yangu zaidi na zaidi,â anasema.
Anaeleza kuwa mwaka 2013 alipata hasara ya mamilioni ya fedha baada ya ubora wa mazao kupimwa na kuonekana upo kwenye kiwango cha 48 badala ya 51 inayotakiwa, hivyo alijikuta katika wakati mgumu kwa kuwa
aliyumba kibaishara kutokana na mtaji wake kukata.
Maziku anasema ilimlazimu kwenda kukopa benki ili aendelee kufanya biashara.
âNilipata hasara kubwa ambayo hadi leo hii bado ninalipa deni nililokopa benki ingawa pia fedha kutoka katika biashara zingine inzozifanya zinaendelea kuifanya biasahara hii kuendelea kuwapo,âanasema mfanyabiashara huyo wa kimataifa.
Kila biashara haikosi vikwazo, Maziku anataja vikwazo wanavyokumbana navyo kuwa ni mtaji mdogo alionao.
Analia na ukiritimba unaofanywa na benki mbalimbali ambazo ili kupata mkopo wanahitaji dhamana kubwa kuliko uwezo wa mfanyabiashara, jambo linalokwamishaukuaji wa biashara.
Anataja kikwazo kingine kuwa ni ukiritimba uliopo kwenye vyama vya
ushirika ambapo hupanga bei zisoendana na ya soko la dunia.
Anasema hali hiyo inawafanya wafanyabiashara wengi kushindwa kufikia
malengo.
âWakati mwingine wafanyabiashara wenzetu huturudisha nyuma kimaendeleo⦠huwa tunawanunulia mazao kwa makubaliaono ya kulipa baadaye, badala yake hutoroka na fedha,â anasema.
Pamoja na mambo mengine, anataja mafanikio aliyoyapata kupitia biashara hiyo kuwa ni kumiliki kampuni mbili ambazo ni GEFU Agromart Company Limited na Lyone investment Company Limited ambazo
zimeajiri wafanyakazi watano akiwamo ofisa rasilimali watu, mhasibu, katibu muhtasi, mwanasheria na meneja mwendeshaji wa
shughuli za kampuni.
Mafanikio mengine ni kwamba ameweza kujenga nyumba ya kuishi, kumiliki usafiri na kupata fursa ya kusafiri kwenda nchi mbalimbali kuhudhuria makongamano na maonyesho ya biashara ya mazao, jambo
ambalo limemkutanisha na watu wengi maarufu hivyo kujikuta akipanua wigo wa biashara yake kimataifa.
Kwa sasa Maziku anatarajia kufungua kampuni ya ujenzi ili kuweza kutoa ajira kwa vijana wengi zaidi wa Kitanzania.
âPia nina mpango wa kufungua kiwanda cha kuzalisha juisi, mafuta ya alizeti, mifuko ya plastiki na maji ya kunywa.
Kiwanda hiki nitakifungua kwa kushirikiana na wawekezaji kutoka nje ili nizidi kukuza uchumi wa Tanzania,â anasema.
Anasema kwa kuwa ana uwezo wa kusaidia jamii, haoni shida kutoa fedha zake kuwasaidia wasiojiweza wakiwemo yatima.
âKidogo nilicho nacho huwa nakitoa na kwa wenye mahitaji maalumu lakini huwa sipendi kujitangaza,â anasema mfanyabiashara huyo.
Maziku anawashauri vijana wenzake kuwa na uthubutu kama aliokuwa nao yeye, aliiona fursa akaichangamkia na hadi sasa amefikia
katika hatua nzuri.
âVijana tusibweteke, vikwazo ni vingi lakini hatupaswi kukata tama. Hata
waliofanikiwa kama akina Mo Dewji hawakuanzia juu. Walipambana na uzuri ni kwamba wafanyabiasahara wakubwa kama Mo si wachoyo, huwa wanajitoa kusaidia wengine kwa kuwapa ushauri wa kibiasahara
Recent Comments