WAKULIMA wa zao la korosho wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma msimu huu wataendelea kuuza zao hilo kwa mtindo wa soko holela badala ya mfumo wa stakabadhi ghalani.
Hali hiyo inatokana na vyama vya msingi vya mazao ambavyo ndiyo mawakala wa ukusanyaji wa korosho kukosa sifa za kukopesheka na vyombo vya fedha.
Ofisa Kilimo, Mifugo na Ushirika wa wilaya hiyo Chiza Marando, alimweleza mwandishi wa habari hii mjini Tunduru juzi kuwa, katika misimu miwili iliyopita wakulima wa wilaya hiyo wamekuwa wakiuza korosho zao kwa mtindo wa soko holela ambapo na msimu wa mwaka huu hali itakuwa kama hiyo kutokana na vyama vya msingi kukosa sifa za kukopa fedha benki.
Mtaalamu huyo wa kilimo alisema katika msimu wa mavuno wa mwaka 2012/13 zao hilo lilikumbwa na tatizo la soko hali iliyofanya korosho za wakulima wa wilayani humo kuuzwa chini ya bei dira iliyowekwa na hivyo kupata hasara. Wakulima na vyama vya msingi vya mazao 17 vimepata hasara.
Vilikopa fedha ili kutoa malipo ya awali kwa wakulima waliokuwa wamekusanya korosho zao chini ya mfumo wa stakabadhi ghalani kuingia katika madeni.
Alisema vyama hivyo hadi sasa vinadaiwa na benki ya NMB Sh bilioni 2.6 ikiwa ni fedha walizokopa na riba inayokuwa mwaka hadi mwaka, na kwamba kiasi hicho kingeweza kuwa zaidi ya hapo lakini serikali imeingilia kati na kuanzisha mazungumzo baina ya vyama na benki ili riba isiongezeke.
Marando alisema serikali wilayani humo imeshachukua hatua kadhaa ili kuviondolea madeni vyama hivyo na hatua iliyopo sasa limefikishwa ngazi ya taifa kuona namna inavyowezekana ili kuwanusuru wakulima na kuuza korosho zao kwa bei ya chini na kwa mfumo ambao tayari ulishapigwa marufuku na serikali.
Akizungumzia uzalishaji Marando alisema mwaka huu wamekadiria kuvuna zaidi ya tani 950 ikiwa ni tani 150 zaidi ya mavuno ya msimu uliopita.
Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on.
Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments