WAKULIMA wa tumbaku katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, wameitaka Serikali kuhakikisha inadhibiti tabia ya makampuni yanayonunua zao hilo katika maeneo mbalimbali kwa kutumia fedha za kigeni.
Walisema, wakulima wengi hawana uelewa wa kutosha kuhusu thamani ya fedha hizo za kigeni na ndiyo sababu wanapohitaji kuzitumia inakuwa vigumu kwao, jambo linalowalazimu kuwatafuta watu waliosoma ambao nao huhitaji fedha ili kuwasaidia.
Hali hiyo, inatokana na wakulima wengi kutofahamu mabadiliko ya fedha za kigeni zinazolipwa na makampuni yanayonunua tumbaku na mazao mengine ya wakulima yanayozalishwa kwa wingi katika wilaya hiyo.
Mmoja wa wakulima wa kijiji cha Matepwende, Abdallah Ngonyani alisema, makampuni kutumia fedha za kigeni, hususan Dola kuwalipa wakulima ni sawa na kuwaibia kwa kuwa wakulima wengi wanaoishi maeneo ya mashambani huwa hawaji na kiwango cha kubadilisha fedha cha wakati huo.
Mbali na hilo alisema huchukua muda mrefu hadi kufika mjini kufuata huduma za kibenki. Ni kwa msingi huo aliiomba Serikali kuanzia msimu huu wa 2015/2016 ikomeshe hali hiyo kwani inawarudisha nyuma wakulima wengi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Ali Mpenye alisema, tayari ofisi yake imeshawaandikia barua watendaji wa vijiji na kata kuwajulisha kwamba hakuna anayeruhusiwa kununua mazao kutoka kwa wakulimakwa kutumia fedha za kigeni.
Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on.
Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments