NA,ANKO G

Mwigizaji Mkongwe wa Bongo Movie Hashim Kambi Amefariki Dunia. Taarifa Hii Imethibitishwa Na Muigizaji Madebelidai kupitia ukurasa wake wa Instagram. “Kila La Kheri Mzee Wangu ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ (R.I.P)”
Kambi amekuwa na mchango chanya katika ukuaji wa tasnia ya uigizaji hapa nchini ambapo alipata nafasi ya kuigiza Filamu Kama Vile: Simu Ya Kifo, Binti Nusa, Babu Seya n.k
Vilevile Kambi amaweahi kuwa mchezi wa mpira wa miguu katika Klabu kubwa Tanzania ya Young African Sport Club (Yanga)
Wakati huohuo Mwanamuziki Spack amefariki dunia akiwa nyumbani kwake Chanika jijini Dar es Salaam leo Aprili 27, 2026.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na baadhi ya majirani zake sambamba na meneja wake Melefti, ambaye amesema chanzo cha kifo bado hakijajulikana.
Spack atakumbukwa katika nymbo kama vile Maumivu (2024),Maisha Safari (feat. Tunda Man & Asala),Nalia,Usiniache,Nachechemea (feat. Badria),Nasubiri,Jeraha La Moyo (feat. Z Anto),Mtima Wangu,Tangu Nitoke Jela,Binadamu Wabaya.
Kuondoka kwa wakongwe hawa ni simanzi na pigo kubwa kwa watanzania na mashabiki wa Bongo Movie na Bongo Freva.
Hakika hili ni pengo kubwa Simamia tv inatoa pole kwa kila mmoja aliye guswa na misiba hii.