Siku za hivi karibuni yalifanyika mashindano ya Miss Ngara ambayo yalifanyika katika Ukumbi wa Morland uliopo Ngara Mjini mkoani Kagera.
Katika hali isiyo ya kawaida mshindi wa kwanza inasemekana kuwa alitokea Mwanza. Mshindi wa pili alitokea Bukoba na mshindi wa tatu alitokea Ngara Mjini.
Wananzengo wanajiuliza ni vigezo gani vilitumika kupata washindi ambao wanatoka nje ya Wilaya ya Ngara na kama yalikua mashindano yanayoihusu Wilaya ya Ngara ama lah?
Kwanza kabisa shindano lilikosa radha halisi ya kuwa ni shindano linalowakilisha Wilaya ya Ngara kwani lilionekana ni shindano la Morland Hotel. Shindano hilo halikutoa nafasi kwa kila kata kutafuta washiriki. Zoezi hilo lilifanyika ndani ya Morland Hotel tangu mwanzo mpaka mwisho hali ambayo ilipelekea watu wanao ishi katika kata nyingine nje ya kata ya Ngara Mjini kutojua kinacho endelea na wengine wengi mpaka sasa hawajui kama kulikua na shindano la Umiss.
Ndipo simamia.com imejipa muda wa kuzungumza na baadhi ya wadau wa Ngara juu ya shindano hilo ambapo mtazamo wao ni kuwa shindano hilo halikupaswa kupewa jina la miss Ngara. Kwa kuwa shindano hilo liliandaliwa na kuchakatwa na Morland Hotel, likafanyika pale pale hotelini kwa siri, na hata waliotangazwa kama washindi kupangwa na wahusika, basi shindano lingepewa jina la Miss Morland. Shindano hili liliandaliwa kutanga huduma na uwepo wa morland Hotel.
Maoni ya wadau wengi walitamani mchakato uanzie ngazi ya kata kisha washindani kutoka kila kata na ndio wakutane Morland au ukumbi wowote kwa ajili ya kutafuta washindi wa Wilaya ya Ngara. Kkwa kushindanisha washiriki kutoka kata zote za Wilaya, shindano kufanyika eneo moja ndiyo maana ilipelekea washiriki ambao wanatoka nje ya wilaya ya Ngara.
Tafiti ya simamia.com imebaini kuwa kiu ya wanangara mpaka sasa wanatamani shinano lirudiwe na kutoa nafasi kwa kila kata kushiriki kwa kuweka vituo vya kutafuta washiriki na kwa kila makao makuu ya Kata ili kuweka radha halisi ya Miss Ngara na hata wale wanao tokea familia masikini ambao hawana uwezo wa kulipa nauli kufika Morland Hotel waweze kujaribu bahati zao. Shindano lilitangazwa kusaidia mabinti wajitafute, wajulikane na waweze kushinda zawadi nono. Unasaidiaje mrembo anayetoka kwenye kaya masikini kushiriki katika shindano ambapo hakupewa hata habari kuwa kulikua na shindano la urembo. Kama shindano limedhamilia kuiwakilisha Wilaya ya Ngara, basi liandaliwe kingara Ngara na mkoani aperekwe yule aliyeshinda na sio kupanga na kudanganya kuwa ameshinda huku aliandaliwa. Miss Ngara awakilishe uhalisi wa Ngara na sio kuwakilisha biashara ya mtu flani.