Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema kuwa atafurahi sana kama Kanisa Katoliki litamtangaza Mwl. Julius Kambarage Nyerere kuwa Mtakatifu kutokana na jinsi alivyopigania usawa wa kijamii enzi za uhai wake. Rais Museveni aliyasema hayo jana katika ibada maalum iliyofanyika katika Kanisa la Namugongo katika maadhimisho ya Siku ya Nyerere ambayo huadhimishwa kila mwaka Juni Mosi. Museveni alisema kuwa Mwl. Nyerere alijitolea sana kupigania haki na usawa katika nchi mbalimbali lakini ikiwa ni pamoja na kuhakikisha nchi nyingine za Afrika zinakuwa huru kutoka kwenye unyonyaji wa kikoloni. Mei 13, 2005 Papa Benedict XVI alimtangaza Mwl. Nyerere kuwa ni Mtumishi wa Mungu (Servant of God) ikiwa ni hatua ya kwanza kuelekea kuwa Mtakatifu. Rais Museveni aliyekuwa akizungumza mbele ya ujumbe kutoka Tanzania na Kenya alisema pia, licha ya Mwl. Nyerere kupigania usawa na haki, lakini alichukia pia utengano ndio sababu alitaka kuona Afrika Mashariki ikiungana. Kwa mujibu wa sheria za Kanisa Katoliki (Canon Law 1187) mtu hutangazwa kuwa Mtakatifu akiwa ameshafariki. Kwa maneno mengine ni kwamba, haiwezekani mtu kuwa Mtakatifu akiwa yupo hai.
Kwa jina anaitwa Shaban Rashid Said Kisleu na ni mhariri hapa Simamia Media Group.
Natumaini mtafurahishwa na yake nitakayowaletea na mtaendelea kufatilia mitandao wa Simamia.com
Kumfikia, tuma email SimamiaTeam@gmail.com
Ameeleweka Nyerere Fahari ya Tz
Ameeleweka Nyerere Fahari ya Tz