NYIMBO nyingi za Bongo Fleva kwa sasa zinabebwa na ubora wa video ambayo msanii anaiÂfanya. Hapa unaweza kukuta wimbo wa kawaida ambao hata haueleweki lakini inatumika gharama kubwa kuhakikisha video yake inakuwa ya kiwango kikubwa.
Suala hilo limewafanya wasanii wengi Bongo kufukuzana na hali hiyo, jambo ambalo limesababisha baadhi yao kuchukua mawazo ya video za wasanii wenzao na kuyaingiza kwenye video zao, yaani kukopi na kupesti.
Awali, suala hilo lilianza kama utani hivi lakini kwa sasa limejichimbia mizÂizi na kukomaa. Idadi ya wasanii ambao wanapesti mawazo ya wenzao katika video zao ni kubwa kuliko kipindi cha nyuma.
Mwanzoni kabisa gazeti hilihili la ChamÂpioni, liliibua na kuonyesha jinsi msanii DiaÂmond alivyorudia mawazo ya wasanii wenÂgine hasa wale wa Ulaya kwenye video ya nyimbo zake. Alianza na Make Me Sing kisha Kidogo na sasa kamalÂizia na Fire ambayo video yake inÂafanana na ile ya Jason Derulo iitÂwayo Swalla.
Baada ya msanii huyo kuyafanÂya hayo, hivi karibuni mwanadaÂda anayekimbiza kwenye game ya muziki huo, Vanessa Mdee âVee Moneyâ naye kaamua kupiÂta mulemule yaani kakopi kisha kupesti katika mkwaju wake mpya wa Kisela ambao amÂempa shavu pacha wa Kundi la P-Square, Paul Okoye.
Kisela ya Vee Money inÂafanana na ile ya Energy iliyofanywa na Keri Hilson wa Marekani, lakini tofauÂti ni miaka, wakati Kisela haina hata wiki mbili tangu iachiwe yaani JuÂlai 10, mwaka huu, EnÂergy ya Keri sasa inagota mwaka wa nane tangu iachiwe kwake Desemba 13, 2009.
Championi Jumatatu linakuletea baadhi ya maeneo ambayo Vee Money aliyesikika kisanii kupitia Ngoma ya Closer, ameiga kutoka kwenye video ya Energy.
Keri Hilson â EnergyÂ
MAZINGIRA YA VIDEO NZIMA
Hapa ndipo tatizo la kukopi na kupesti alilofanya Vee Money linapoanza, haihitaji elimu ya chuo kikuu kutambua kwamba mazingira ya vidÂeo zote mbili yanafanana yaani ile ya Kisela na EnÂergy.
Vee Money ametemÂbelea mawazo ya Keri Hilson ya kutengeneza video katika mazingira ya âgymâ (sehemu ya kuÂfanyia mazoezi kwa wanaÂmasumbwi) ambapo mwanzo mwisho video hiyo imeshutiwa eneo hilo kama ilivyo ya Energy.
UWANJA WA NGUMI
Hili pia ni eneo lingine ambalo Vee MonÂey âdizaini fâlan amelipestishaâ kwenye vidÂeo yake ambapo mwanzoni tu mwa video yake anaonekana yuko kwenye ulingo wa ngumi jambo ambalo hata Keri amelifanya katika video yake na hata kukaa kwenye viti vinavyowekwa kwenye kona ya mabondia.
Ukifuatilia kwenye video zote mbili ya Keri na Vee Money, utabaini kuwa wasanii wote wametumia eneo la ulingo kwa asilÂimia kubwa katika kushutia video zao.
KUPIGA PUNCHING BAG
Vee Money ameendelea kuonyesha kuwa hakutumia nguvu kubwa kuwaza kuitengeneza video yake hiyo hata kama atakuwa ametumia fedha nyingi kuitenÂgeneza.
Eneo lingine ambalo linamuonyesha Vee Money amekopi na kupesti ni kwenye kipengele hiki ambapo kule kwa Keri anaonekana kupiga âpunching bagâ kwa ajili ya kujiandaa na pambano lake jambo hilohilo linafanywa na Vee Money kwenye video yake ya Kisela. Hapo utaona kabisa kuwa amekopi tu tukio la mwenzake kisha kulihamishia kwake.
KUPIGA SPEED BAG
Kukopi kamwe hakutamuacha salama Vee Money kwani vipengele alivyovitumia kwenye wimbo wake ndivyo vinamhukumu mwenyewe, ukiitazama vizuri Video ya EnÂergy kuna sehemu inamuonyeÂsha Keri akipiga âspeed bagâ na ukirudi kwa Vee Money naye mwanÂzoni alikuwa akiÂfanya hivyo kabla ya baadaye kuja kufundishwa na Paul Okoye jinÂsi ya kukitumia kifaa hicho.
Recent Comments