Siku 3 baadae Alikiba alitoa wimbo wake mpya alioupa jina la Seduce Me ambapo saa moja baadae Diamond kupitia instagram yake alipost picha ya mtu anaecheka kwa kebehi ikatafsiriwa kama vile ameudharau wimbo wenye, jioni yake Diamond nae akawatangazia mashabiki wake kuhusu kuachia wimbo mpya aliowashirikisha wasanii wote walio chini ya label ya Wasafi uliopewa jina la Zilipendwa na kilichofuatia hapo ni ushindani mkubwa wa mashabiki ambao wamekuwa wakitupiana maneno.
Hata hivyo suala la Diamond kutoa wimbo ni kama vile halijapokelewa vizuri na wasanii wengine ambao wanaona lengo lake ni kujaribu kuuzima wimbo wa Alikiba na wengi ukifuatilia utagundua wamechagua upande wa Seduce Me badala ya Zilipendwa. Yameibuka maneno zaidi kuhusu namna ambavyo label ya Wasafi imekuwa na tabia ya kutoa nyimbo siku msanii yeyote mkubwa akiachia wake, kana kwamba wanataka wao tu ndio wasikike msanii mwingine asiwe juu yao.
Ninavyomfahamu mimi Diamond ni mtu ambaye yuko humble sana ukiongea nae, na nyuma ya pazia huwasaidia wasanii wengi tu wanapokuwa na matatizo. Hili suala la ugomvi wa kujaribu kuwabania wasanii wengine wasisisike inajulikana wazi ni management yake imekuwa ikilisukuma. Ushauri wangu kwake ni kuwa ajihadhari na hii tabia na kubali kwamba ushindani ni mzuri kwenye muziki lakini isifikie hatua ya kutaka kumharibia msanii mwenzake. Asiruhusu mameneja wake Babu Tale na Sallam kumuingiza kwenye ugomvi na wasanii wengine ambao asilimia kubwa Diamond anawaheshimu kama kaka zake, atambue nguvu ya umma iliyotumika kumtetea Alikiba inaweza kuhamia kwenye kazi zake nyingine na kumshusha kabisa.
Ni hayo tu.
Recent Comments