BARAZA la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limetenga Sh bilioni moja kwa ajili ya kudhamini mikopo inayotolewa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa vyama vya Kuweka na Kukopa vya Bodaboda (Saccos) nchi nzima na watakaoanza kufaidika ni Saccos ya Waendesha Bodaboda Dar es Salaam (Dabosa).
Mkopo huo unalenga kuwezesha waendesha bodaboda wa Dar es Salaam kukua, kuinuka kimtaji na kumiliki bodaboda zao kwa kuwa wengi si za kwao bali wameajiriwa.
Katibu Mtendaji wa NEEC, Bengâi Issa alisema hayo baada ya kutiliana saini ya makubaliano ya kudhamini NSSF kutoa mikopo kwa Dabosa itoe mikopo kwa wanachama wake.
âFedha hizo za kudhamini mikopo hii zitawekwa kwenye akaunti ya mfuko huo,â alisema na kuongeza kuwa watatoa mkopo kwa riba ya asilimia 9.32 na Dabosa itatoza kwa wanachama wake kwa asilimia 12.3.
Alifafanua zaidi, Issa alisema mpango huo ni wa kitaifa wenye lengo la kuwezesha wananchi kiuchumi, hivyo watashirikiana na mfuko huo kuwapatia mafunzo ya utawala bora, kuweka akiba na ujasiriamali. âMafunzo yameshaanza kutolewa Dar es Salaam na yataendelea kufanyika pia katika mikoa mingine nchini,â alisisitiza.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhani Dau alisema mikopo hiyo ni njia ya kuwezesha vijana kuondokana na tatizo la ajira linalowakabili.
âMfuko umejiweka tayari kutoa mikopo hii, lakini jambo la msingi ni kwa vijana waweze kufanya kazi kwa bidii na kuwa waaminifu katika biashara zao ili waweze kurejesha mikopo,â alisema Dk Dau.
Mkurugenzi huyo mkuu aliwaelezea waendesha bodaboda kuwa mfuko unatoa huduma za jamii zikiwemo za mafao ya ajali na mafao ya afya, hivyo wanaweza kujiunga na kunufaika nayo wakati wanaendelea na shughuli zao.
Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji, Omari Issa ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais Utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), alisema programu ya kuwezesha bodaboda ni moja ya mambo yaliyomo katika BRN.
âBaraza limeondokana na mfumo wa zamani wa kutoa mikopo kwa wananchi moja kwa moja na sasa inadhamini taasisi za kifedha kutoa mikopo kwa wananchi,â alisema.
Alisema wanafanya hivyo na Benki ya Posta, TIB, NSSF na watashirikiana na taasisi nyingine ili kuendelea kuwafikia wananchi wengi zaidi. Mwenyekiti wa Dabosa, Said Kagomba alisema chama chao ni cha vijana wa jiji la Dar es Salaam kina wanachama 439. Kinondoni wako wanachama 135, Ilala ni 163 na Temeke ni 141.
âLengo ni kuinua, kustawisha na kuboresha hali ya maisha yetuâ na mpaka sasa wamekusanya kiasi cha Sh milioni 24.7,âalisema Kagomba.
Recent Comments