Limao hutumika sana na watu Tanzania wengine huwa wanatumia kama kiungo kwenye mboga pia wengine hutumia kuweka kwenye supu, chai na vinywaji vingine ili kupata ladha tu lakini ya kutambua kuwa matumizi ya limao yana tija kwa afya ya binadamu hasa linapotumiwa asubuhi. Unaweza tumia limao kama juisi kila asubuhi au ukatumia lenyewe kama lenyewe na ikakuletea tija hizo.
Faida za malimao au ndimu
A) Husaidia katika mfumo wa umeng’ enyaji wa chakula hivyo husaidia kulainisha choo, inashauriwa kuwa watu wanaosumbuliwa na choo hasa kukosa choo au kupata cho kigumu wanashauriwa kutumia limao kila asubuhi ili kuondosha adha hii.
B) Hutunza na kulinda kinywa hasa afya ya meno yako, ambapo matumizi ya limao kila asubuhi husaidi kung’ arisha na kusafisha meno hasa kwa wale wenye meno yenye rangi ya njano weka vitone kadhaa wakati unapokwenda kupiga mswaki.
C) Ina mchango mkubwa katika utunzaji wa nywele, inashauriwa mtu kuchukua maji ya limao na kupaka nywele zake asubuhi ili kymuzipa nguvu na afya na kwa watu ambao wana nywele chache limao hujaza nywele pia huzing’ arisha na kuzipa ule muonekano wake halisi.
D) Pia limao hupunguza uzito katika mwili, wataalamu huwa wanasisitiza kwamba inatakiwa asubuhi mtu atumia glasi ya maji iliyo na ndimu au limao pamoja na asali ili kusaidia ule mfumo wa kuyeyusha mafuta mwilini ambapo hii hupunguza uzito wa mwili.
E) Hutuepusha dhidi ya uvimbe wa figo hii ni kwa sababu limao wmau ndimu ina virutubisho vingi ambavyo huzuia figo kuvimba.
F) Pia Limao huchuja sumu kwenye ini na figo ambapo husafisha vijidudu vinavyopelekea bacteria wabaya na kuondosha sumu mwilini.
G) Pia limao huongezea kinga mwilini ambapo limao huongezea nguvu zile seli zinakinga mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali hivyo ni vyema kutumia kila asubuh ili kulinda miili yetu.
@Ventas Malack
naomba mniunge kwenye grup lenu