Serikali ya Saudi Arabia inapanga kupunguza matumizi kwa sababu ya bei ya mafuta kuporomoka – pato kubwa la nchi hiyo linatokana na kuuza mafuta nchi za nje.
Waziri wa Fedha, Ibrahim Alassaf, alisema baadhi ya miradi iliyokuwa imepitishwa, sasa huenda ikaahirishwa.
Hakutoa maelezo zaidi lakini alisema bajeti ya sekta muhimu kama afya na elimu haitoathirika.
Serikali ya Saudi Arabia imetabiri nakisi katika bajeti ya mwaka huu ya karibu dola bilioni 40, lakini wadadisi wa kimataifa wanafikiri huenda ikawa kubwa zaidi.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako
Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on.
Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments