Recent Comments

MWENYEKITI WA UVCCM KATA YA NGENGE ATOA MPIRA KUIMARISHA WANAFUNZI KIMICHEZO

By Simamia Ngara May 17, 2024

NA,ANKO G.

Mwenyekiti wa umoja wa vichana chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kata ya Ngenge wilaya ya Muleba mkoani Kagera Maximilian M Winchlaus ametoa mpira katika shule ya Sekondari ya Kishuro iliyopo katika kata hiyo kwaajili ya maandalizi la bonanza la michachezo ya kukutanisha shule za Sekondari katika kata hiyo litakalo fanyika mwezi Julai 2024.

Aidha mwenyekiti huyo amefika katika shule ya Sekondari Kishuro na kutoa mpira utakao wasaidia wanafunzi wa shule hiyo kufanya mazoezi kwaajili ya kujiandaa na bonanza la michezo linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni kwa kukutanisha shule za Sekondari za kata ya Ngenge kimichezo.

Vilevile katika mahohiano na simamia.com Bw. Winchlaus amesema “Baada ya kuwa nafanya Bonanza kwa kuzikutanisha shule za Sekondari zilizomo katika Kata ya Ngenge kila mwaka, Mwaka huu nimeanza na kuwatafutia mipira ya mazoezi ili kufikia mwezi wa saba ambapo Bonanza litafanyika vijana wetu wawe na mazoezi ya kutosha. Ndipo niliweza kushirikisha Mdau wa michezo ndani ya wilaya ya Muleba Ndg. Wakili Muhalila nae akaniunga mkono na tayari amenipatia mpira mmoja wa Kishuro Sekondari na taratibu za kupata mpira Ngenge Sekondari zinaendelea”.

Hata hivyo mwenyekiti huyo ameiambia simamia.com kuwa amekua akiandaa Bonanza kila mwaka lengo ikiwa ni kukutanisha vijana pamoja, kubadilishana mawazo na kuimarisha vipaji walivyonavyo.

Pia Mwenyekiti huyo amemalizia kwa kuiambia simamia.com kuwa ataendelea kuandaa na kutengeneza program zinazo waunganisha vijana kwa nafasi aliyonayo kama mwenyeki wa vijana wa chama hicho.