Recent Comments

NGARA ACHENI KUCHOMA MISITU

By Mwafrika Sep 6, 2023

NA, ANKO G

Biashara ya miti ni miongoni mawa biashara zinazo fanyika katika wilaya ya Ngara ambapo watu huwekeza katika biashara hiyo kwaajili ya kujipatia kipato.

Upandaji wa miti ni kwaajili ya kuzalisha mbao, miti ya kujengea ambapo miti hiyo huuzwa ndani ya wilaya ya Ngara na na mingine ikosafirishwa nje ya wailaya hiyo.

Vilevile kumekua nabia ya baadhi ya watu ambao huchoma misitu hasa kipindi cha kiangazi ambapo majani yamekauka jambo linalopelekea kuteketeza mashamba ya miti ambayo watu wamewekeza.

Vilevile uchomaji huo wa misitu unasababisha hasara kubwa kwa watu wanao wekeza kwenye biashara hiyo jambo linalo warudisha nyuma kimaendeleo.

Hata hivyo simamia.com imefika kijiji cha Ibuga kata ya kambanga na kushuhudia mashamba ya miti/misitu ikiwa imeteketezwa na moto.

Pia uchomaji wa misitu wa aina hii unasababisha hasara kwa wafanya biashara wanao wekeza kwenye miti/ misitu kwani ni mazao yanayo chukua muda mrefu mpaka kuvuna na kujipatia pesa.

Hivyo basi simamia.com inawaasa wakazi wa wilaya ya Ngara kuachana na tabia ya kuchoma misitu kwani jambo hili husababisha hasara kwa wafanya biashara na uchafuzi wa mazingira.