Biharamulo: Nyota ya Kung’ara, Mungu ni Mwema

By Baraka Bitariho Sep 8, 2023
Dkt Gresmus Sebuyoya - Nyota ya Jamii yaendelea Kung'aa
BIHARAMURO NA NGARA MNATAKA MUNGU ATUPE NINI?
Wakati nikiwa mdogo, nikisoma Sunday School na watoto wenzangu tuliimba Wimbo wa “JIWE WALILOKATAA WAASHI NI JIWE IMARA, LIMEKUWA JIWE KUU LA PEMBENI”
Sasa nimekuwa mkubwa ndio naelewa maana ya Wimbo huo. Msomaji wa www.simamia.com  na SimamiaTV, katika pita pita za kuandaa kipindi cha Simamia Profile nikaona ni vyema nikushirikishe habari ya ndugu yetu Daktari Gresmus Sebuyoya.
Katika kipindi cha Simamia Profile (Sima 100% Profile), tunaleta habari ya yale yanayotokea kwenye jamii. Katika kipindi hiki cha Sima 100% Profile, yanayoletwa ni yale yanagusa jamii na kama jina la kipindi linavyojieleza, yakiwa yamefanyika kwa asilimia 15, 25, ama 210, kwetu yote ni tunayathamini kwani Muumba alitupatia uwezo tofauti tofauti na hamna mtu aliyekuwa kamilifu. Na ndio maana hata jina letu, Simamia, tulilichagua kwa kuwa tunatambua hamna mtu aliyekua kamilifu, 100%, na hata yale tunayoyaleta yatafurahisha baadhi ya watu huku inaudhi wengine. Cha maana ni kutambua mchango wa kila mmoja wetu katika jamii zetu.
Ni kinyume cha taratibu zetu kutoa maksi ila tunakuachia wewe unayefatilia programs na makara zetu uamue.
Dkt Gresmus Sebuyoya – Nyota ya Jamii yaendelea Kung’aa
Na haya ni baadhi ya tunayofahamu kwa kijana huyu wa kitanzania, msomi na mchapa kazi kweli kweli. Miaka iliyopita nilikutana nae Wilayani Ngara akiwania kuteuliwa kugombea Ubunge kupitia Tiketi ya Chama Cha Maendeleo CHADEMA.
Baadae nilisikia ametia nia, akawa miongoni mwa waliopiitishwa na CCM huko Biharamulo kugombea Ubunge. Kwa bahati mbaya wakati wa Utawala wa Hayati JPM jina la Gresmus Sebuyoya likanyofolewa kichwa ya kuwa aliongoza kwenye kura za maoni!.
Dhuruma hiyo haijatoka mionyoni mwa Wana CCM wa Biharamulo.
Habari njema ni kwamba nyota yake bado inaendelea kung’ara. Kwa picha na bango hapo juu sasa anaitwa Rais wa Madaktari wa Hospitali za Makanisa.
Kwa sasa Gresmus Sebuyoya ni Mganga mkuu wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Biharamulo DDH.
Tunamuombea uwajibikaji mwema, na Mungu ambariki. Binafsi nimefurahi kuona kuwa nyota iliyofunikwa kipindi flani, bado inang’ara na kuhudumia jamii kwa moyo mkunjufu. Kwa hiyo naombeni tuungane na kusema Congratulations Dr. Gresmus Sebuyoya.
Na  pia
Pongezi nyingi kwa Baba Askofu Severine Niwemugizi.