Haya wanetu kuanzia ngazi ya kitongoji mpaka Tiafa mpo nyie vipi mnasemaje huko mambo yapo shwari au mlewe tena 2025 mmalizie kazi zilizobaki?
Hakuna kitu kibaya kama mtu upewe nyumba nzima uishi na ufanye kila kitu alafu mwisho wa siku ufanyiwe tathmini ya namna ulivyoishi mhh hapa lazima ujiwekee mazingira mazuri kama kutoa uchafu na kulima mapori yanayozunguka nyumba ili wageni wakose lakusema.
Au mnasemaje waungwana au niseme kama waliwaonea kuwapa nchi nzima na badala yake mngegawana kidogo na majirani nao ili muwe mnapeana kasuhirikiano eeh.
Wanangu wananchi msijali maisha ndio haya haya hata wakija tena 2030 mambo ni yaleyale tu yaani kiufupi ahadi zetu si mnazijua mambo yakutoa asali na maziwa kwenye mito ila tukipita aah tunakula kuku kwa mrija.
Bandugu msijali natania tu ila na nyie majirani nao mmezidi sasa yaani sasaivi mnacheza ngoja ya mwenzenu bila hata ya kibwebwe aah au ngoma imekolea sana mmeshimdwa kujizuia.
Ila yote kwa yote niseme tu kuna watu wanalia wakiwa na njaa ila wakishiba wanasahau kila kitu na kesho wakipatwa na njaa wanalia tena kiufupi maisha yaendelee ila sisi makapuku tuanapenda masiha mazuri hayo menì0gine hayatuhusu na ujumbe huu atauelewa mwenye uelevu pekee.
Recent Comments