Recent Comments

UTUMIAJI WA KUMBI ZA TURUBAI KWENYE SHEREHE NGARA

By Mwafrika Sep 12, 2023

NA,ANKO G

Kwa kawaida imezoeleka Turubai zikitumika kwenye kufunika mazao, magari,kuezeka nyumba n.k lakini wilayani Ngara hali ni tofauti Turubai kutumika kutengeneza ukumbi kwaajili ya sherehe kama vile Harus, Sendoff, Kipaimara, Ubatozo, Misiba na sherehe zinazo fanana na hizo.

Kutokana na hali ya uchumi mpamoja na kudumisha mila na sesturi za Kihangaza na Kishubi baadhi ya watu hawafanyii sherehe zao katika kumbi maalumu kwaajili ya sherehe badala yake hutengengeneza kumbi majumbani mwao kwa kutumia Turubai.

Uandaaji wa kumbi hizo huanza na kutundika miti ya kushika Turubai hizo ambapo hutumia miti aina ya Mikaratusi na kisha kutundika Turubai juu ya miti hiyo ambapo Turubai hizo huzuia watu wa nje kuona kinacho endelea ndani, kuzuia jua pamoja na Mvua.

Vilevile kumbi hizo kutumika kwa muda mfupi na kisha kuondolewa baadha ya sherehe kuisha ambapo huondolewa.

Hata hivyo asilimia kubwa hukodi Turubai hizo kati ya Tsh1000 na Tsh2000 kwa watu ama vikundi vinavyo kodisha Turubai huku miti ikinunuliwa kati ya Tsh2000 na Tsh3000.

Watu wengi hudhani kuwa kutengeneza ukumbi wa aina hiyo huokoa gharama licha ya kuwa gharama za ujenzi wa kumbi hizo hazitofautiani sana na kumbi maalumu za sherehe.

Pia simamia.com imefika kwa Ibrahim Isack amabae ni mkazi wa kijiji cha Mrukukumbo kata ya Kabanga wilayani Ngara tumekuta akiwa na sherehe ya kumpokea mama mkwe wake ambapo amejenga ukumbi nyumbani kwake ukumbi wa Turubai kwa kushirikiana na kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo.

Hivyo basi simamia.com imebaini kuwa ukumbi wa namna hiyo huathiri matumizi ya Camera kwani Turubai zinazo tumika kujengea kumbi hizo huakisi mwanga ambao huathili matumizi ya Camera katika uchukuaji wa picha mnato na picha mjongeo na kuwa na muonekano usio faa ukilingani na kumbi maalumu za sherehe.

Utumiaji wa kumbi za aina hii unaweza usifae sana kipindi cha mvua kali hasa zile zinazo ambatana na upepo kutokana na uimara wa ujenzi unao fanywa.

Vilevile simamia.com inashauri watu kutumia kumbi maalumu kama wakihitaji kupata picha nzuri licha ya kumbi za Turubai kuonekana bei ikiwa nafuu ukulinganisha na ukumbi maalumu wa sherehe.